loader
Picha

Amunike atoa sababu kufungwa Stars

Kocha wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars Emmanuel Amunike amesema Tanzania imefungwa na Senegal kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) kwa sababu wachezaji hawana uzoefu.

Juni 23 Taifa Stars ilicheza na Senegal kwenye uwanja wa June 30 mjini Cairo ikafungwa mabao 2-0.

Amunike leo amewaeleza waandishi wa habari mjini Cairo kuwa, Senegal ni timu nzuri na ina uzoefu wa kutosha kulinganisha na Taifa Stars.

"Tanzania haijafuzu michuano hii kwa miaka 39... kikubwa ni uzoefu wa wachezaji wetu, hata Uganda Afcon iliyopita hawakuwa vizuri lakini sasa mnawaona wamekuwa wazoefu,"amesema.

Amesema mechi ijayo dhidi ya Kenya itakuwa ngumu lakini hana mashaka kwa kuwa ni timu wanayofahamiana.

"Sisi na Kenya wote ni Afrika Mashariki, tunazungumza laugha moja kiswahili, tunafahamiana vizuri. Naamini itakuwa derby nzuri sana," amesema.

Leo Rais John Magufuli amesema, wachezaji wa timu ya soka ya Taifa 'Taifa Stars' wasikate tamaa kwa kuwa kufungwa mabao 2-0 na Senegal si matokeo mabaya sana.

Ametoa mwito kwa Watanzania wawape moyo wachezaji wa Taifa Stars kwa kuwa kufungwa kwao ni kufungwa kwa Watanzania na kushinda kwao ni ushindi kwa Watanzania.

"Kwa hiyo wao wakakazane, wakajitume zaidi, na sisi tuendelee kuwaombea...kwa hiyo tusimame tuendelee kuwasaidia na kuwaombea"ameyasema hayo akiwa Vijibweni wilayani Kigamboni, Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa maghala na mitambo ya gesi ya kampuni ya Taifa Gas.

"Na mimi nina uhakika huo mwanzo sio mbaya sana, kufungwa tugoli tuwili tu, kwa timu ambayo inaongoza katika Afrika, ambao wachezaji wote wale wanacheza nje, mimi nilifikiri tuendelee kuwapa moyo"amesema Magufuli.

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Afrika ...

foto
Mwandishi: Zena Chande, Cairo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi