loader
Picha

Msuva hataki kwenda Simba

Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Simon Msuva amesema hayupo tayari kucheza Simba SC wala Yanga SC kwa sasa.

Msuva yupo Misri na timu ya soka ya Taifa 'Taifa Stars' inayoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).

Ametoa msimamo huo baada ya kuwepo tetesi kuwa anatarajia kusajiliwa Simba SC msimu ujao.

"Mimi kwa sasa akili yangu ipo kimataifa zaidi, sina mpango wa kurudi Yanga wala kwenda Simba," amesema Msuva.

Msuva anacheza El Jadida ya Morocco na amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba.

KOCHA wa timu ya taifa ya Algeria, Djamel Belmadi ana ...

foto
Mwandishi: Zena Chande, Cairo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi