loader
Picha

Wanafunzi 250 wajengewa sekondari

WANAFUNZI zaidi ya 250 kutoka kata ya Luhaita, Myangayanga na Mateka Halmashauri ya Mji Mbinga mkoani Ruvuma, wanatembea kilometa 40 kila siku kwenda na kurudi shule kutokana na shule ya Sekondari Mateka kutosajiliwa licha ya ujenzi wake kukamilika.

Kutokana na kadhia hiyo, wazazi wa kijiji cha Mateka wameiomba serikali kuharakisha usajili wa shule ya sekondari Mateka ili kuwaondolea usumbufu watoto kwenda shule nyingine huko. Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mateka, Libaba Gervas alisema, kuna tatizo la muda mrefu la ukosefu wa sekondari na wazazi na halmashauri wamejitolea kujenga shule moja kuwapunguzia adha watoto wanaochaguliwa kuanza masomo ya sekondari kwenda kusoma maeneo mengine.

Libaba alisema, kata ya Mateka kuna watoto zaidi ya 200 wanaosoma shule mbalimbali za sekondari, lakini wana kero kubwa ya kutembea umbali mrefu, jambo linalochangia baadhi yao kukatisha masomo na wanafunzi wa kike kupata ujauzito kutokana na vishawishi wanavyokutana navyo njiani wakati wa kwenda na kurudi shule. Alisema, wazazi na halmashauri wametumia gharama kubwa kujenga shule hiyo na itakuwa vyema serikali ikawaharakishia usajili wake ili watoto waanze kusoma na kuchochea taaluma.

Festo Nombo, Diwani wa kata hiyo alisema, watoto wao wanapata tabu kubwa ya kutembea zaidi ya kilometa 20 kufuata masomo kwingine. Alisema jambo hilo linachangia baadhi ya wanafunzi kutofanya vizuri darasani kutokana na uchovu wanapofika shule, watoto wa kike kukatisha masomo kwa kupata mimba na hivyo kuishia njiani kabla ya kufika kidato cha nne.

Msimamizi wa ujenzi huo, Anton Ndunguru alisema, walipokea Sh milioni 87.5 kutoka Tamisemi kupitia Halmashauri ya Mbinga Mji na wametumia Sh milioni 77 kujenga vyumba vitano na kufanya ukarabati wa vyumba vingine viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu.

Ndunguru alisema, changamoto kubwa ilikuwa ni kukosa nguvu za wananchi walioshindwa kufanya kazi za kujitolea hivyo kutumia kiasi kikubwa cha fedha ambapo kama wangeshiriki ujenzi fedha zilizotumika zingekuwa kidogo. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mbinga, Grace Quintine aliishukuru serikali kutoa fedha kujenga shule za sekondari na msingi.

Alisema kwa sasa mpango ni kuhakikisha shule hiyo inapata usajili wake ifikapo Januari, mwakani ili ianze kutumika na kusisitiza kuwa, ujenzi wa shule hiyo umetokana na kero wanayoipata wanafunzi wa kata ya Mateka, Myangayanga, na Luhaita ambao wanalazimika kwenda shule ya Mbambi kufuata masomo.

KIWANGO cha utabiri wa hali ya hewa nchini kinazidi kukua ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Mbinga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi