loader
Picha

Kijana anavyotumia urefu kupata fedha

MAISHA ya mwanadamu yanaweza kubadilika ghafla na kumbadilisha kabisa mtu kimaumbile tofauti na alivyokuwa awali kinyume kabisa na matarajio ya wazazi waliohusika kumleta duniani na kuwa mtu wa tofauti katika jamii. Haya ndiyo yaliomkuta kijana Julius Charles mwenye umri wa miaka 24.

Alipozaliwa mpaka alipofika umri wa miaka 14 alikuwa na maumbile ya kawaida, yaliofanana na ndugu na marafiki zake lakini ghafla alianza kubadilika kimaumbile na kurefuka isivyo kawaida alipofikisha miaka 15.

Anaamini urefu wake ni fursa kubwa ya kuitangaza nchi yake na kustawisha maisha yake binafsi. Ukiomuona lazima utake kumtazama zaidi kwa kuwa, urefu wake kwa sasa ni tofauti kabisa na alipokuwa na umri wa chini ya miaka 14. Kimo chake kimemfanya kila anayemuona ama amshangae au atake kupiga naye picha au kutaka kumsalimia angalau asikie sauti yake.

Ana urefu wa mita 2.19 na kilo 110. Amezidiwa kidogo na Mtanzania na mchezaji mashuhuri wa mpira wa kikapu (basketball) anayeishi Marekani hivi sasa, Hashim Thabit mwenye urefu wa mita 2.21 na uzito wa kilo 119. Sina uhakika kama anayendelea kurefuka na huenda akampita Hashim, lakini unaweza kusema kwa sasa miongoni mwa hazina ya watu warefu nchini, Julius ni mmoja wao.

Nimefanikiwa kuzungumza naye Jumatano wiki hii katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), maarufu Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, katika barabara ya Kilwa, kujua historia yake.

Nilipomsalimia kwa kulazimika kuinua shingo sana ili anione vizuri wakati najitambulisha kwake na kuomba kuzungumza naye, nilishtuka kusikia anavyozungumza.

Sauti yake ni tofauti kabisa na umri wake mdogo wa miaka 24, akizungumza unaweza kufikiri ni mwanaume mwenye zaidi ya miaka 45 kutokana na uzito wa sauti yake, lakini inaendana na umbo lake kubwa ingawa ni kijana mdogo bado.

Historia ya maisha yake ina sehemu zenye uchungu mwingi, lakini kwake yeye zimekuwa ni za kawaida japo moja ya kutoonana na mama yake tangu aliporefuka sana, inamuumiza kichwa.

“Nilizaliwa hospitali ya Bugando Mwanza mwaka 1995. Nimesoma shule ya Msingi Mlimani huko Mwanza na baadaye nikapata ufadhili wa kusoma katika sekondari ya Lord Baden Powell Memorial iliyopo Bagamoyo, Pwani na nikamaliza elimu hiyo katika shule ya Mesack Open ya Dar es Salaam,” anaeleza Julius.

Ni mchezaji wa mpira wa kikapu, mchezo huo umempa mafanikio makubwa baada ya kupata ufadhili wa kusoma bure elimu ya sekondari lakini pia kwenda nchini Marekani Januari hadi Mei mwaka huu na sasa anakamilisha vigezo vichache vitakavyomuwezesha kurudi nchini humo kuendelea na masomo.

“Napenda sana mpira wa kikapu lakini zaidi napenda kusoma. Nilipokwenda Marekani ilikuwa ni kwa ajili ya kutembea, lakini sasa kuna mambo nafuatilia, nikikamilisha nitarudi huko rasmi kusoma, napenda kusoma, nikisoma hata mchezo wa kikapu nitaucheza vizuri,” anasema.

Julius ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya watoto saba. Tangu alipopata ufadhili kuja Dar es Salaam kusoma elimu ya sekondari akiwa na miaka 14 na kuanza kurefuka, hajaonana ana kwa ana na mama yake kwa kuwa hakuwahi kupata likizo.

Sasa anajiandaa kwenda Mwanza kukutana na mama yake mzazi anayesikia habari za mwanae kwa simu, picha, redio na kupitia ndugu zake.

“Nazungumza na mama kwa simu karibu kila siku, anajua nimerefuka sana ila hajaniona, ninajiandaa kwenda, sijui itakuwaje akiniona”. Baba yake pia hakubahatika kumuona katika muonekano huo mpya alionayo kwa kuwa alifariki miaka 10 iliyopita Julius akiwa na miaka 14 kabla hajaanza kurefuka kusiko kawaida.

Alipoanza kurefuka alijiona kuwa anakuwa mtu wa tofauti, alijaribu kuuliza huku na kule na baadhi ya watu walimueleza kuwa ni maumbile yanatokea na huenda kwao kuna mtu mrefu kama yeye.

Wataalamu wa afya waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotaja majina, wanasema mabadiliko yanaweza kutokea katika mwili wa mtu wakati wowote kwa sababu ya kurithi, ajali na magonjwa. Julius anasema haumwi na alikwenda hospitali mwanzoni na kuambiwa hana tatizo lolote la kiafya.

Awali alikuwa hatoki ndani kwa hofu ya watu kumuona, baadaye akatiwa moyo na familia anakoishi kwa baba yake mdogo Mbande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Hana taarifa kama kwao kumewahi kuwa na watu warefu kama yeye.

Kijana huyo mwenye ndoto kubwa ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa, anasema awali watu walipokuwa wanamshangaa na kumnyooshea vidole, alijisikia vibaya.

Baadaye aligundua kuwa jinsi alivyo ni fursa adimu kwa kuwa watu wa namna yake wapo wachache Tanzania na hata duniani na kuanza kujikubali.

“Nilianza kupiga picha na watu kwa fedha. Nilijikubali na kujisikia fahari sana kuwa hivi. Sasa najiona kawaida hata kama watu wananishangaa kwa namna gani,” anasema Julius ambaye katika maonesho hayo

KIWANGO cha utabiri wa hali ya hewa nchini kinazidi kukua ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi