loader
Picha

Waziri- Chezeni msiwe legelege

WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amewataka watu kushiriki michezo ili kujenga afya bora zitakazowawezesha kufanya kazi kwa bidii na kuinua uchumi wa nchi.

Hayo aliyasema mjini hapa wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Kimataifa ya Olimpiki iliyofanyika wilayani Chato mkoani Geita na kushirikisha zaidi ya watu 700.

Siku ya Olimpiki huadhimishwa Juni kila mwaka, lakini nchini imefanyika kitaifa jana kutokana na Juni 23, tarehe iliyopangwa awali kuingiliana na Michezo ya Shule za Msingi (Umitashumta) na hivyo kufanyika jana.

Alisema taifa linatakiwa kuwa na watu wenye afya njema, wazee kwa vijana, ambao wataweza kulijenga taifa kwa kuchapa kazi kwa bidii bila ya kusumbuliwa na magonjwa na matatizo mengine yanayosababishwa na afya duni.

Alisema kamwe huwezi kujenga nchi kama wananchi wako watakuwa na afya legelege, hivyo aliwataka kufanya mazoezi na kushiriki katika michezo ili kuwa na nguvu.

“Kamwe huwezi kujenga uchumi kama watu wako watakuwa na afya legelege, hivyo jitahidini kushiriki michezo,“ alisema Kalemani wakati akizungumza na washiriki wa maadhimisho hayo ya Siku ya Olimpiki.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi, ambao ndio waandaaji wa maadhimisho hayo nchini kwa kushirikiana na mkoa husika alisema huu ni mwaka 125 tangu kuanzishwa kwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC).

Aliwashukuru viongozi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na ile ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kwa kushirikiana nao vizuri hadi kufanikisha tamasha hilo la maadhimisho ya Siku ya Olimpiki.

Katika maadhimisho hayo, watoto wenye umri mdogo zaidi wa kike na kiume, Lukumai Mrisho (3.5) na Gift Munawe (3) kila mmoja aliondoka na zawadi ya fedha taslimu Sh 50,000 na mwanaume na mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi, Anicet Magayane (62) na Bertha Henry (53) nao kila mmoja aliondoka na kiasi kama hicho cha fedha.

Mbali na hao, pia mtoto mlemavu, Ramadhani Fredy mwenye umri wa miaka minne naye aliondoka na kitita cha Sh 50,000 baada ya kumaliza mbio za kilometa 2.5.

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Chato

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi