loader
Picha

Tanzania kubangua 60% korosho zake

TANZANIA katika kipindi cha miaka minne kuanzia sasa itakuwa na uwezo wa kubangua asilimia 60 ya korosho zote zinazozalishwa nchini.

Kwa sasa, inazalisha tani 313,000 na lengo ni kuzalisha tani 600,000 kuanzia mwaka 2023/2024.

Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Francis Alfred jijini Dar es Salaam alipokuwa anazungumzia Siku ya bidhaa za kimkakati kwenye Maonesho ya 43 Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

Alisema kubangua korosho wenyewe kutasaidia kukamata masoko ya nchi mbalimbali ikiwemo katika ukanda wa Afrika Mashariki, kwani kwa sasa soko la nje kwa korosho zisizobanguliwa ni katika nchi mbili pekee za Vietnam na India, hivyo kuwepo kwa ufinyu wa soko kutokana na kuuza korosho ghafi.

Aidha, alibainisha kuwa uzalishaji wa korosho kwa sasa ni takribani tani 313,000 kwa mwaka na wamejiwekea lengo ifikapo mwaka 2023/2024 kuzalisha korosho tani 600,000 na sambamba na hilo wanahitaji kiasi kikubwa kubanguliwa nchini kwani kwa sasa asilimia 24 pekee ya korosho inayozalishwa inabanguliwa nchini.

Alisema katika maonesho hayo wamepata kampuni za kununua korosho ikiwemo kampuni ya Sunshine na wadau mmoja mmoja na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamepata soko kubwa la wananchi kununua na kwenda kuuza, kwani wao wamekuwa wakiuza kwa bei nafuu hasa zile zilizobanguliwa na serikali.

Alibainisha kuwa, awali kiasi kikubwa kilikuwa kikiuzwa nje kwa korosho zisizobanguliwa, lakini sasa wanasisitiza katika uwekezaji wa kubangua korosho nchini na matumizi ya bidhaa za

Mkoa wa Pwani umebaini kuwa maonesho ya bidhaa zinazozalishwa viwandani ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi