loader
Picha

Rais Madagascar atabiri ubingwa

RAIS wa Madagascar, Andry Rajoelina amesema ni fahari kwa taifa hilo baada ya timu ya taifa kufuzu robo fainali za michuano ya kombe la mataifa Afrika, Afcon.

Madagascar inayoshiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza imezidi kuushangaza umma wa wapenda soka baada ya kufuzu hatua ya mtoano na juzi kutinga robo fainali kwa kuwatoa Congo DR kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida.

Rais huyo ambaye alitoa ndege kwa mashabiki kwenda Misri baada ya timu hiyo kufuzu hatua ya mtoano ameiambia BBC: Tupo tayari kuthibitisha kwamba hii ni timu ya ushindi.” Alisema sasa wamefuzu robo fainali, watakwenda mbali na kushinda taji. “Tutakwenda mbali mpaka kushinda taji,” alisema. Akizungumzia hatua hiyo, kocha wa Madagascar, Nicolas Dupuis alisema mechi ilikuwa ngumu dhidi ya Congo yenye uzoefu mkubwa zaidi.

“Tulifanya kwa kadri tunavyoweza na kuendelea kuandika historia nzuri naamini tutaendelea kufanya vizuri.” Mechi nyingine zilizochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita mabao ya Youcef Belaili, Riyad Mahrez na Adam Ounas yaliipeleka Algeria robo fainali kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Guinea.

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: ANTANANARIVO, Madagascar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi