loader
Picha

Mikel Obi akiri kucheza fainali za mwisho

NAHODHA John Mikel Obi amesema fainali za mwaka huu ni za mwisho kwake akiamini kuwafanya Wanigeria kumkumbuka na kuamini uwepo wake kwenye kikosi ni moja ya kufanya kikosi hicho kuwa na mafanikio.

“Ni safari ya kufurahisha kwangu kwenye timu ya taifa,” Mikel mwenye umri wa miaka 32 aliiambia BBC Sport. “Hakuna shaka kuwa kushinda taji Afrika Kusini ni jambo kubwa sana na ndio ninalotaka kuwasaidia kuwasaidia vijana wadogo kwenye timu kufikia ndoto zao,” alisema. “Miaka 13 nadhani inatosha, nimeshinda mataji, nimekuwa na wakati mzuri, nadhani ni wakati kwa vijana wote kuendelea.”

“Nipo hapa Misri kuwasapoti vijana, na kuhakikisha wanakuwa kwenye mstari sahihi.” “Nadhani uwepo wangu mara zote ni muhimu kwao, ninaamini naweza kumaliza na taji.” Mikel amecheza mechi 89 kwa Nigeria, akicheza kwenye kombe la dunia mara mbili na kuisaidia Super Eagles kushinda taji la Afrika mwaka 2013. Pia aliisaidia Nigeria kumaliza ya tatu kwenye michuano ya Afcon mwaka 2006 na 2010.

Amecheza mara mbili kwenye michuano inayoendelea sasa Misri lakini alikosa mechi ya hatua ya 16 kutokana na kuwa majeruhi ambapo Nigeria ilikata tiketi ya kucheza robo fainali na Afrika Kusini kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Cameroon. Sasa Mikel anawania kuwa sehemu ya kikosi cha Nigeria kinachowania taji la nne. “Kama nipo fiti ningependa kucheza robo fainali, lakini alihitaji kufanya haraka,” aliongeza.

“Ninaamini kama tunaweza kucheza nusu fainali, nitakuwa tayari na kuisaidia timu kama nitahitajika.” Mchezaji huyo aliyecheza fainali ya kombe la dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2005, mchezaji wa zamani wa Chelsea anaamini ana mchango wake katika mafanikio ya taifa hilo la Afrika Magharibi.

“Kama tutakuwa tayari kushinda hapa, nitafurahi sana, kisha wanaweza kuendelea kutoka hapa.” Alikuwa pia miongoni mwa wachezaji watatu wa Nigeria waliozidi umri walioshinda medali ya shaba kwenye michezo ya Olimpiki Rio mwaka 2016.

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi