loader
Picha

Misri yaweka historia

KUTOKANA na kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Afrika Kusini kwenye uwanja wa kimataifa wa Cairo Jumamosi iliyopita, Misri inaungana kwenye orodha ya timu mwenyeji zilizotolewa hatua ya mtoano ya michuano hiyo.

Tangu kuwekwa kwa utaratibu wa hatua ya mtoano (badala ya nusu fainali kwa timu nane) mwaka 1992 idadi ya timu shiriki ilipokuwa 12, timu sita tu zilizoondolewa hatua ya kwanza ya mtoano kwenye michuano.

Mafarao wameweka historia ya kuwa timu ya kwanza mwenyeji kuondolewa mapema katika mpango mpya wa raundi ya 16 ya michuano hii inayofanyika kwa mara ya kwanza ikishirikisha timu 24. Wenyeji Senegal walipoteza kwa bao 1-0 kwa Cameroon kwenye robo fainali mwaka 1992. Mwaka 2000 waandaaji wenza Ghana walikumbana na jinamizi hilohilo dhidi ya Afrika Kusini.

Angola ilipoteza kwa matokeo kama hayo kwa Ghana mwaka 2010. Mwaka 2012, waandaaji wenza wote Equatorial Guinea na Gabon walipoteza kwenye robo fainali, Equatorial Guinea ikichapwa mabao 3-0 na Ivory Coast na Gabon kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Mali. Mali ilimtoa mwenyeji tena mwaka mmoja baade kwa kuifunga Afrika Kusini kwa mikwaju wa penalti mwaka 2013.

Orodha ya wenyeji waliotolewa mapema 1992 Senegal 0-1 Cameroon (robo fainali), 2000 Ghana 0-1 Afrika Kusini (robo fainali), 2010 Angola 0-1 Ghana (robo fainali). 2012 Equatorial Guinea 0-3 Ivory Coast (robo fainali) 2012 Gabon 1-1 (4-5 penalti.) Mali (robo fainali). 2013 Afrika Kusini 1-1 (1-3 penalti.) Mali (robo fainali) 2019 Misri 0-1 Afrika Kusini (mtoano). Mwaka 2012, Equatorial Guinea na Gabon walishirikiana kuandaa fainali.

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi