loader
Picha

Upanuzi bandari Kisumu wakamilika kwa 90%

MAANDALIZI ya kuzinduliwa kwa bandari ya Kisumu nchini humu yamepamba moto baada ya kukamilika kwa asilimia 90 ya marekebisho yanayohusu upanuzi wa bandari hiyo ambapo kiasi cha shilingi za Kenya bilioni tatu zilitumika.

Taarifa kutoka vyanzo vya habari vilivyo karibu na Ikulu ya Kenya vinasema kuwa Rais Uhuru Kenyatta atatembelea mji wa Kisumu ambako ni nyumbani kwa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga kukagua maendeleo ya ukarabati huo wa bandari. Ziara hiyo inatajwa kuwa itafanyika ndani ya wiki hii ambapo mwezi ujao wa Agosti ndio muda uliowekwa kukamilika kwa ujenzi wa bandari hiyo na kuzinduliwa kwake kunatarajiwa kuwa Agosti 15 . Upanuzi wa bandari ya Kisumu ulianza rasmi Mei mwaka huu na inatarajiwa kuanza kufanya kazi kabla ya mwaka 2020.

Ukarabati huo ni moja ya mipango ya serikali ya kuimarisha miundombinu ya mji wa Kisumu, hali itakayochochea ukuaji wa uchumi katika mji huo. Miongoni mwa miundombinu inayotarajiwa kukamilika mwaka huu na kupaisha uchumi wa mji wa Kisumu ikiwa ni azma ya serikali kuimarisha uchumi wa watu wa Kisumu ni pamoja na mradi wa uchimbaji wa mafuta, ujenzi wa meli ya abiria na mizigo, pamoja na ukarabati wa bandari ya Kisumu.

SERIKALI ya Uganda imesema itatuma Dola za Marekani milioni 60 ...

foto
Mwandishi: KISUMU, Kenya

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi