loader
Picha

Wanaosambaza picha za ajali waonywa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe ametoa onyo kwa watu wenye tabia ya kupiga picha zinapotokea ajali na kuzituma mtandaoni.

Ametoa onyo hilo jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga miili ya wafanyakazi watano wa kampuni ya Azam Media Limited waliokufa kwa ajali ya gari jana, mkoani Singida.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa hili ni onyo la mwisho na hatua kali zitaanza kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria dhidi ya wanaoendeleza vitendo hivyo.

“Watanzania naomba tuendeleze utamaduni wa utu bila kutumia sheria, naomba acheni tabia za kuchukua picha za ajali na kutuma mitandaoni,” aliongeza.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni amewaeleza waombolezaji kuwa, Jeshi la Polisi tayari limeanza uchunguzi kuhusu ajali hiyo na kwamba, dereva wa lori lililogongana uso kwa uso na basi la wanahabari hao ameshakamatwa.

“Wito wangu ni wananchi endeleeni kuwa makini mtumiapo vyombo vya moto barabarani ili kuokoa maisha maisha yenu na ya watu wengine,” amesema.

Rais John Magufuli amemuagiza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi