loader
Picha

Mkwasa amtetea Amunike

KOCHA wa zamani wa timu ya Soka ya Taifa, Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema licha ya Shirikisho la Soka nchini, TFF,,kusitisha mkataba na Emmanuel Amunike kuna haja ya kutazama upya mfumo wa uendeshaji wa mchezo huo.

Akizungumza jana, Mkwasa aliyewahi pia kufundisha Yanga alisema uamuzi huo huenda usiwe dawa ya kukifanya kikosi cha Stars kufanya vyema kwa siku za usoni kutokana na kwamba kuna makocha wengi wamepita lakini bado timu hiyo inafanya vibaya.

Mkwasa ametoa maoni hayo, ikiwa ni siku moja imepita baada ya TFF na Amunike kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba, kuokana na kuboronga kwenye fainali za Afcon 2019 zinazoendelea nchini Misri.

Stars iliyoshiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39, iliishia hatua ya makundi kwa kupoteza mechi zote. “Sawa Amunike ameachishwa kazi, lakini lazima tujiulize tunakosea wapi, ilhali tumepata kuwa na makocha wengi lakini bado tumeendelea kufanya vibaya, niwaombe wenye mamlaka ya kuendesha soka kuna kila sababu ya kutazama upya mfumo wetu wa uendeshaji wa mchezo huu, nakujiuliza maswali wanaofanya vizuri wanautaratibu gani?” alisema Mkwasa.

Mkwasa ambaye amewahi kucheza Yanga na Stars enzi zake, alisema anaamini uamuzi huo umetokana na presha ya mashabiki baada ya kufanya vibaya kwenye michuano ya Afcon.

Alisema, Tanzania ina wachezaji wenye vipaji vikubwa vya kucheza mchezo huo, lakini bado utaratibu haujawa wezeshi kuwafanya wachezaji wawe inavyotakiwa. Kocha Amunike, raia wa Nigeria amejikuta akiachishwa kazi kutokana na ubovu wa rekodi zake toka aliporithi majukumu ya kukinoa kikosi hicho kutoka kwa mtangulizi wake Salum Mayanga. Amunike katika mechi zake 10 alizokiongoza kikosi hicho ameshinda mechi mbili, sare mbili na kupoteza mechi sita.

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi