loader
Picha

Kubwa kuliko ya Yanga yaahirishwa

WIKI ya wananchi ya Yanga ‘Kubwa Kuliko’ iliyokuwa ifanyike Julai 27, mwaka huu imesogezwa mbele kupisha mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) kati ya Taifa Stars na Kenya unaotarajiwa kufanyika Julai 28 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga ilipanga kufanya sherehe za wiki ya wananchi siku hiyo ambapo itatambulisha jezi na wachezaji waliowasajili kwa msimu mpya wa Ligi Kuu. Akizungumza na gazeti hili jana Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema wanaweza kubadilisha tarehe na kusogeza hadi mwezi ujao kupisha maandalizi ya timu ya taifa.

“Tutasogeza mbele wiki ya wananchi kwa sababu ya mchezo wa Chan, ili kutoa nafasi kwa timu ya taifa, tutatangaza baada ya kupanga tarehe,”alisema. Alisema mabadiliko hayo ya tarehe hayawezi kubadilisha mipango yao ya maandalizi, wanaendelea kujiandaa hadi watakapotangaza tena tayari kwa sherehe hizo za wiki ya wananchi maalumu kwa ajili ya kutangaza kikosi kipya cha msimu.

Mwakalebela alisema wachezaji wote waliosajiliwa wameanza maandalizi ya msimu mpya katika kambi yao ya Morogoro wakitarajiwa kukaa huko hadi Julai 30, mwaka huu. Yanga tayari imeshakamilisha usajili wa wachezaji 29 watakaoanza nao msimu ujao huku 14 wakiwa wapya na 15 wa zamani. Ingizo jipya ni Abdulazizi Makame, Farouk Shikalo, Muharami Issa, Metacha Mnata, Ally Mtoni, Juma Balinya, Mustapha Seleman, Mapinduzi Balama, Maybin Kalengo,Ali Ali, Lamine Moro, Sadney Khoetage, Patrick Sibomana na Issa Bigirimana.

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi