loader
Picha

Tanzania kupanda daraja AfDB

BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inatarajia kuipandisha daraja Tanzania kutoka katika hadhi ya kunufaika na Mfuko wa Maendeleo wa Benki (ADF) hadi kuwa na hadhi itakayoiwezesha Tanzania kuweza kupata rasilimali fedha zaidi kupitia dirisha la African Development Bank (ADB) la Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Endapo Tanzania itafanikiwa kupandishwa hadhi, nchi itaweza kunufaika na ongezeko la fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kutoka Dola za Marekani milioni 350 kwa mwaka hadi Dola za Marekani milioni 812 kwa mwaka.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo, Dk Alex Mubiru alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Katika mazungumzo hayo, Dk Alex alieleza kuwa hatua hiyo ya kupandishwa hadhi ama kupandishwa daraja, inatokana na uchumi wa nchi kufanya vizuri na kuwa na deni himilivu.

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru alisema kuwa benki hiyo inajivunia kufanya kazi na Tanzania ambayo ni miongoni mwa nchi waasisi wa Benki hiyo.

Katika mazungumzo yao, Dk Mpango alieleza kuwa serikali inajivunia kufanya kazi pamoja na AfDB kwa kuwa benki hiyo imekuwa na masharti rafiki katika upatikanaji wa mikopo.

Dk Mpango alisema kuwa benki hiyo ina mtazamo chanya katika maendeleo ya watu na kuwa dira katika mipango ya maendeleo.

Aliahidi kushirikiana nao vyema katika kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, Mpango aliipongeza benki hiyo kwa kukubali kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara ya mzunguko Dodoma (kilometa 110.2) kwa kiwango cha lami na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma (Msalato)

Rais John Magufuli amemuagiza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi