loader
Picha

Simba yaahidi 'sapraizi' kumrithi Okwi

NI rasmi Simba imeachana na mshambuliaji wake wa siku nyingi, Emmanuel Okwi na wekundu hao wamesema wanatarajia kushusha mrithi wake wakati wowote.

Mpaka sasa wachezaji waliopelekwa katika usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ni 26 huku Mtendaji Mkuu Crescentius Magori akisema kazi imekwisha.

Akizungumza na gazeti hili jana, Magori alisema wamemaliza kazi kubwa na kilichobaki ni mchezaji mmoja ambaye ataziba nafasi ya Okwi na itakuwa ni ‘sapraizi’ kwa mashabiki wao.

“Asilimia kubwa ya wachezaji waliohitajika tayari wamekamilika labda mchezaji mmoja wa kimataifa anaweza kuongezwa kuziba nafasi ya Okwi, tutamtaja baadaye baada ya mambo kukamilika,” alisema.

Mshambuliaji wa Nkana, Walter Bwalya ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuwa wamemalizana na wekundu hao wa Msimbazi.

Magori alisema sababu za kuachana na Okwi aliomba kuondoka kwenda kutafuta fursa nyingine baada ya kumaliza mkataba wake.

Mchezaji huyo anahusishwa na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini huenda akaenda kuungana na mchezaji mwingine James Kotei aliyesajiliwa hivi karibuni baada ya kumaliza mkataba wake Simba.

Mpaka sasa Simba imesajili wachezaji wapya 10 ambao ni Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Gervas Fraga, Traitone da Silver, Kenned Wilson, Sharaf Shoboub, Francis Kahata, Ibrahim Ajibu, Deo Kanda na Wilker Henrique.

Katika hatua nyingine, Simba imemtambulisha rasmi beki Gadiel Michael baada ya kujiunga nao kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Yanga. Gadiel aliyetoka kuitumikia timu ya taifa katika michuano ya Afrika alimaliza mkataba wake kwenye timu yake ya zamani alikotumikia misimu miwili akitokea Azam FC.

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi