loader
Picha

Robo fainali za ‘kufa’ mtu Afcon

MECHI za robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, Afcon, zinaanza leo ambapo Senegal itamenyana na Benin. Mechi ya leo haitabiriki ingawa Senegal inapewa nafasi kubwa ya kushinda.

Timu hizo hazijawahi kukutana kwenye Afcon. Senegal ilikata tiketi ya robo fainali kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda na Benin iliifunga Mauritania kwa mikwaju ya penalti 4-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1. Robo fainali nyingine leo itazikutanisha Nigeria na Afrika Kusini. Nigeria ilitinga hatua hiyo baada ya kumfunga bingwa mtetezi Cameroon mabao 3-2 na Afrika Kusini iliwaondoa wenyeji Misri kwa bao 1-0.

Timu hizo ziliwahi kukutana mwaka 2000 mjini Lagos kwenye nusu fainali ya michuano hiyo na Nigeria iliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Zikakutana tena mwaka 2004 kwenye hatua ya makundi na Nigeria ilishinda kwa mabao 4-0, leo kama itaendeleza ushindi ama Afrika Kusini itapindua meza, itajulikana. Mechi nyingine ya robo fainali itachezwa kesho kati ya timu ngeni kwenye michuano hiyo Madagascar na Tunisia.

Timu hizi pia hazijawahi kukutana kwenye Afcon, Madagascar ilitinga hatua hiyo kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya Congo DR baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida.

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi