loader
Picha

Kocha Uganda apata kazi Misri

KOCHA Mfaransa Sebastien Desabre amepata kazi mpya, ikiwa ni siku moja baada ya kuachana na kibarua cha Uganda. Amerejea kwenye klabu na kusaini mkataba wa miaka miwili na Pyramids FC ya Misri.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 42, ameondoka Uganda baada ya kutupwa nje ya michuano ya Afcon kwenye hatua ya mtoano kwa kufungwa bao 1-0 na Senegal Jumamosi iliyopita. Itakuwa mara ya pili kwa Desabre kupata timu Misri, alishawahi kufundisha Ismaily, alipoondoka na kwenda Uganda Desemba 2017.

Pia aliwahi kufanya kazi na Asec Mimosas ya Ivory Coast, Coton Sport Garoua ya Cameroon, Esperance ya Tunisia, Recreativo Libolo ya Angola, JS Saoura ya Algeria na Wydad Casablanca ya Morocco.

Pyramids inamilikiwa na Mwenyekiti wa Saudi Sports Authority Turki Al Sheikh, ambaye anataka klabu hiyo ishindane na Al Ahly na Zamalek Misri. Jeuri yake ya fedha imeifanya kufuzu michuano ya kimataifa msimu ujao baada ya kumaliza ligi na pointi 70.

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Afrika ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi