loader
Picha

Wawekezaji Ufaransa wana imani na Tanzania

UFARANSA imesema ina imani kubwa na safari ya Tanzania kwenda kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda mwaka 2025 kutokana na kasi ya ukuaji wa uchumi wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Balozi wa nchi hiyo hapa nchini, Frederic Clavier alisema kutokana na hali hiyo wawekezaji wa Ufaransa wameona haja ya kuja Tanzania.

“Ufaransa ina imani kubwa na maendeleo ya Tanzania na kampuni za Kifaransa hazina mashaka katika kuja kuwekeza hapa na kufanya biashara na Watanzania kila zinapokotokeza fursa hizo,” amesema Balozi Clavier.

Alisema biashara kati ya nchi hizo mbili imeongezeka kwa asilimia 30 kwa mwaka jana sawa na dola za Marekani 200.

Balozi Clavier alisema katika kuisaidia Tanzania kukuza uchumi wake na pia kuimarisha ushirikiano, jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania na wa Ufaransa wanatarajiwa kukutana hivi karibuni.

Kwa upande mwingine, alisema Shirika la Maendeleo la nchi hiyo (AFD) limeahidi kuongeza misaada yake kwa Tanzania mpaka kufikia dola milioni 110 katika miradi ya maendeleo katika sekta ya maji, usafirishaji na umeme pamoja na ahadi nyingine ya dola milioni 23.

SHIRIKA la Taifa la Biashara (ZSTC) limesema ni makosa kwa ...

foto
Mwandishi: Regina Mpogolo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi