loader
Picha

Diwani adaiwa kumbaka mtoto

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimemsimamisha nafasi ya udiwani, Diwani wa Wadi ya Mtoni, Hamza Khamis Juma (40) kwa tuhuma za kwenda kinyume na maadili ya uongozi wa chama hicho.

Diwani huyo anakabiliwa na mashitaka mawili ya kutorosha na kumbaka mtoto wa kike wa miaka 16 ambaye yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake.

Akitoa uamuzi huo, Katibu wa CCM Mkoa wa Magharib Kichama Mgei Mussa Haji, alisema uamuzi huo umezingatia kanuni ya Kamati ya Ulinzi na Maadili ya Uongozi ya chama hicho kwa mujibu wa ibara ya 97 (7) ya kanuni ya CCM.

“Kiongozi yeyote ambaye anatuhumiwa anapaswa kuitwa katika kamati ya ulinzi na maadili ya uongozi ya chama hiki, na kupewa nafasi ya kusikilizwa kwa hivyo tulimpa nafasi hiyo na kisha kuchukua maamuzi haya,” amesema.

Katibu huyo wa CCM alieleza kuwa pamoja na kwamba kesi ya mtuhumiwa huyo ipo mahakamani lakini chama kimetoa uamuzi huo kutokana na kuwa hakikubaliani na vitendo hivyo vya udhalilishaji ambapo serikali na chama hicho inavipinga.

“Tunaiachia mahakama ifanye kazi yake endapo mshitakiwa atakua hana hatia atarejeshwa nafasi yake ya uongozi lakini endapo atakutwa na hatia chama kitafuta nafasi yake ya uongozi,” amesema.

Aidha, aliwataka viongozi wengine katika chama hicho kujitambua kuwa wao ni viongozi waliopewa dhamana ya kuwaongoza wananchi katika misingi mizuri na kuepukana na vitendo vya udhalilishaji.

Mshitakiwa huyo Hamza Khamis Juma, amekiri kuitwa na chama chake katika kamati ya wadi na halmashauri ya wilaya hiyo na kupewa nafasi ya kujieleza kuhusiana na tuhuma hizo.

Alieleza kuwa anaheshimu uamuzi wa chama hicho na anasubiri uamuzi wa mahakama na kama ni kweli amefanya kosa hilo hatua iweze kuchukua mkondo wake.

Ilidaiwa na Mahakama ya Mkoa Vuga kuwa Aprili 4, mwaka jana majira ya saa 11:00 alfajiri mtuhumiwa huyo, alimchukua mtoto huyo (jina linahifadhiwa) ambaye hajaolewa, kwa kumtoa kwa Mmanga Mwanyanya na kumpeleka kwenye nyumba iliyopo Mwanyanya, bila ridhaa ya wazazi wake.

Mara baada ya kumtorosha, majira ya saa 11:20 alfajiri, mshitakiwa huyo anadaiwa alimuingilia kimwili ilhali akijua kuwa si mke wake.

Rais John Magufuli amemuagiza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi