loader
Picha

TPB yaikabidhi Serikali bilioni 1.2/-

BENKI ya TPB imekabidhi gawio la Sh bilioni 1.2 kwa serikali pamoja na wanahisa wengine wa benki hiyo.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi gawio, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Dk Edmund Mndolwa alisema gawio hilo limetolewa baada ya Benki ya TPB kufanya vizuri katika kipindi cha mwaka 2017/18.

“Mwaka jana benki imefanya vizuri kwa kupata faida ya Sh bilioni 17, hivyo kuweza kutoa gawio la Sh bilioni moja kwa serikali na Sh milioni 200 kwa wanahisa wake.

“Najisikia faraja kusimamia benki inayoendelea kufanya vizuri miongoni mwa benki takribani 54 zilizopo sokoni hivi sasa. Wanahisa wanaridhishwa na utendaji wa benki kwa kipindi hiki kwani benki ilifanikiwa kupata faida ya Sh bilioni 17.2 kabla ya kodi,”alieleza.

Aidha, Dk Mndolwa aliiomba serikali kutoa vibali vya ajira kwa wakati ili kuboresha utendaji kazi wa benki hiyo.

Alisema sheria ya ajira ndiyo mwiba kwao licha ya uwezo wa kulipa mishahara na mahitaji ya watumishi, lakini mzunguko wa kupata kibali unakwenda kwa kusuasua hivyo waliotaka kuwaajiri wanachukuliwa na benki nyingine.

Awali, Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi alisema benki hiyo imeimarika ukilinganisha na miaka minane iliyopita ambapo ilikuwa katika hali mbaya ya kukatisha tamaa.

Moshingi alisema kwa sasa benki imebadili mfumo wa uendeshaji na kufikia mtaji wa Sh bilioni 82 kutoka Sh bilioni nane zilizokuwepo, huku wakiongeza faida kutoka Sh milioni 800 kwa mwaka hadi kufikia Sh bilioni 12 walizopata mwaka jana.

Akipokea mfano wa hundi kutoka benki hiyo, Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango aliwataka watumishi wa benki zote nchini kutoa huduma bora zenye viwango vya kisasa na kukwepa matapeli ambao wanaweza kujipenyeza kuharibu sifa za benki.

Aidha, Dk Mpango aliahidi kufuatilia suala la kibali cha ajira katika eneo ambalo benki hiyo imekuwa ikikwama, huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza mtaji na watoe gawio kubwa zaidi mwakani.

SERIKALI imetoa ripoti ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi