loader
Picha

TACAIDS, WBC kuelimisha vijana VVU

Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) inatarajia kufikia vijana milioni 15 nchini kuwaelimisha kuhusu Ukimwi na Virusi vya Ukimwi.

TACAIDS kwa kushirikiana na lebo ya muziki ya Wasafi (WCB) imejipanga kufikia vijana hao kupitia tamasha la Wasafi Festival linalotarajiwa kuanza Julai 19 na kupita mikoa zaidi ya minane nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa tume hiyo Jumanne Isango, ameyasema hayo leo wakati anazungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam.

“Kwenye matamasha haya tutatoa elimu ya kujikinga na VVU, dhidi ya unyanyapaa kwa wenye VVU, matumizi sahihi ya kondomu pamoja na kugawa kondomu bure kwa washiriki,” amesema.

Aliongeza kuwa lengo ni kutengeneza taifa lisilo na maambukizi ya VVU, lisilo na unyanyapaa dhidi ya waathirika na vijana wanaoishi maisha salama, na kwamba, matamasha ya burudani yana mchango mkubwa kutimiza malengo hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa WCB ambaye pia ni mwanamuziki wa bongo flava, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema matamasha hayo ni fursa kwake kupata elimu ya masuala ya ukimwi lakini pia kwa vijana wengine nchini ili kuishi maisha salama.

WANAWAKE wenye matatizo ya Fistula nchini wametakiwa kuacha kujifungia ndani ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi