loader
Picha

Tanzania, Misri kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri, Abdel Fattah Al-Sisi, ambapo wametumia fursa hiyo kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi zote mbili kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi.

Mbali na kuzungumzia masuala hayo ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kisiasa, kiuchumi na kijamii, pia Waziri Mkuu amemfikishia Rais wa Misri salamu kutoka kwa Rais wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, mazungumzo baina ya Waziri Mkuu na Rais wa Misri yaliyofanyika jana Ikulu jijini Cairo, ikiwa ni katika siku ya tatu na ya mwisho ya ziara yake ya kikazi nchini Misri.

Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alimaliza ziara yake ya kikazi nchini Misri ambapo aliagwa na Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi wa Misri, Dk Ezz Eldien Abo Setit katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cairo.

Akiwa ziarani nchini Misri, Waziri Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri, Dk Mostafa Madbouly katika siku yake ya kwanza ya ziara yake, ambapo aliwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Misri waje kuwekeza nchini.

Pia, Waziri Mkuu alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo nchini humo ambayo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa makao makuu mapya ya nchi hiyo, mradi wa awamu ya pili ya upanuzi wa mfereji wa Suez na kiwanda kikubwa cha ngozi.

WANAWAKE wenye matatizo ya Fistula nchini wametakiwa kuacha kujifungia ndani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Misri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi