loader
Picha

Waliokula fedha za wastaafu waadhibiwa

MAHAKAMA ya Wilaya Shinyanga imewahukumu kwenda jela mwaka mmoja au kutoa Sh milioni tatu kila mmoja watumishi watatu wa Hospitali ya kanisa la AICT Kolandoto, Manispaa ya Shinyanga kwa kosa la kutafuna Sh milioni 17.5 ambazo ni fedha za wastaafu.

Waliohukumiwa ni Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Dk Elimaliki Katani, Mhasibu Mkuu Samson Masele na aliyekuwa Mhasibu Hamisi Batano. Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Shinyanga Janeth Masesa, mbele ya waendesha mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Shinyanga, Kelvin Murusuri na Sengoka Mndambi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo, alisema watumishi hao wametiwa hatiani kwa kutorejesha serikalini fedha za mishahara ya mtumishi aliyestaafu Lucy Munguli tangu mwaka 2014. “Watumishi hawa wametiwa hatiani kwa matumizi mabaya ya madaraka yao ya ajira kinyume na kifungu Na 31 cha sheria ya Takukuru Na 11 ya mwaka 2017 katika kesi ya uhujumu uchumi Na.03/2017,” alisema.

Hakimu Masesa alisema mishahara ya mtumishi aliyestaafu Lucy Munguli pamoja na fedha ya ruzuku ziliendelea kutumwa na serikali hospitalini hapo tangu Januari 2014 hadi Julai 2015. Hata hivyo, baada ya kusikiliza pande zote, Hakimu huyo aliwaamuru kila mmoja kulipa faini ya Sh milioni tatu au kwenda jela mwaka mmoja.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Shinyanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi