loader
Picha

Butiku awataka Watanzania kutomkatisha tamaa Rais

MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kulinda mali za taifa badala ya kumkatisha tamaa kwani ndiye aliyekabidhiwa kuzisimamia.

Aidha, amewataka viongozi kusimama Katiba na misingi yake kwani hata Rais wa awamu ya kwanza Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake aliwahi kusema taifa linaipuuza. Akizungumza katika kongamano la siku maalumu ya amani katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea Dar es Salaam, Butiku alisema kuna watu waliozoea kutumia vibaya mali za nchi kwa maslahi yao binafsi, hali ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

“Kazi ya serikali ni kukemea wananchi wanaofuja mali za umma na wakati mwingine kuchukua hatua kali ikiwamo kuwashtaki na hata kuwafunga jela hivyo Watanzani wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli katika ulinzi wa amani za taifa.”

“Changamoto zinazotokana na wachache zinatakiwa kufanyiwa kazi, kwani hata watoto unaweza kuzaa wa tabia tofauti wanakuwapo wezi, wahuni au walaghai lakini unatakiwa kuwalea kwa misingi sahihi na kuzingatia maadili mema,” alisema. Alitaja misingi ya amani kuwa ni haki, maendeleo sawa kutokana na mali za nchi, kutii viongozi na kuzingatia katiba.

Akizungumza katika mdahalo huo kuhusu wajibu wa viongozi wa dini katika kuleta amani kwa ajili ya maendeleo ya biashara na uchumi wa viwanda, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema uchumi wa viwanda unahitaji uzalendo na amani, kuweka mbele maslahi ya taifa, kuwapo mapinduzi ya fikra, utaalamu na juhudi na maarifa ili kuhakikisha nchi inafikia uchumi wa kati.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi