loader
Picha

Mbaroni akidaiwa kutaka kumtapeli DC

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Dar es Salaam inamshikilia mkazi wa Chamazi, wilayani Temeke, Omari Chuma (55 kwa tuhuma ya kutaka kumtapeli Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Takukuru, jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Takukuru, Ali Mfuru alidai Omar alijitambulisha kwa mkuu huyo wa wilaya kuwa ni ofisa wa serikali kutoka idara ya usalama wa taifa na kwamba ana taarifa zake mbaya za kiutendaji ambazo anataka kumsaidia kumsafisha.

Alisema baada ya Takukuru kupata taarifa juu ya mtu huyo kutoka vyanzo vyake mbalimbali walizifanyia kazi kwa haraka na kuweka mtego uliomnasa mhusika. Wakati wa mkutano huo wa Takukuru na waandishi wa habari, mtuhumiwa huyo aliingizwa kwenye chumba cha mkutano na kuoneshwa kwa waandishi na alionekana kutaka kuzungumza jambo kabla ya kuondolewa bila ya kusema chochote na wala waandishi kumuuliza swali.

Mfuru alisema kwa kuwa tukio hilo limetokea mkoa wa Pwani, jana mtuhumiwa huyo alipelekwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani kujibu tuhuma zinazomkabili. Aliwataka watu wenye tabia kama hizo kuacha mara moja kwa kuwa ofisi yake imejipanga kuwakabili na kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Takukuru kuwafichua wenye tabia za kihalifu.

Alisema wiki tatu zilizopita Takukuru iliwakamata matapeli sita ambao walikuwa wakishirikiana na maofisa wa Serikali na maofisa wawili wa kampuni za simu kufanya uhalifu. “Mtandao huo wa utapeli unashirikiana na baadhi ya watumishi wa umma na wa kampuni za simu kwa lengo la kupata taarifa za kiongozi wa ngazi za juu serikalini wanayelenga kumtapeli,” alisema.

Mfuru alisema Takukuru imeshaanza kuwafuatilia wafanyakazi wa kampuni za simu na watumishi wa umma wanaoshirikiana na wahalifu na kwamba uchunguzi ukikamilika wahusika watawafikisha mahakamani. Kuhusu namna ambavyo mkuu huyo wa wilaya ya Kisarawe alitaka kutapeliwa, Mfuru alisema kwa sasa hawezi kuweka wazi undani wa suala hilo hadi upelelezi ukamilike.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi