loader
Picha

Dk Shein amtumia salamu za rambirambi Bakhresa

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Makampuni ya Bakhresa, Said Salim Bakhressa kutokana na vifo vya wafanyakazi watano wa Azam Media Limited kutokana na ajali ya barabarani.

Ajali hiyo Jumatatu katika eneo la katikati ya Igunga (Tabora) na Shelui (Singida) ambapo wafanyakazi hao pamoja na madereva wawili waliofariki dunia baada ya basi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari la mizigo wakati wakielekea wilayani Chato kwa ajili ya uzinduzi wa hifadhi hiyo ya Taifa ya Chato-Burigi.

Katika salamu hizo za rambirambi Rais Shein alieleza kuwa amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya ajali hio na kwamba yeye binafsi pamoja na wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania nzima kwa jumla wamejawa na simanzi nzito kutokana na vifo vya wafanyakazi hao.

“Kutokana na msiba huu, natoa salamu za rambirambi kwako Said Salim Bakhressa, ndugu, wanafamilia wa marehemu, marafiki, wafanyakazi wote wa Makampuni ya S.S. Bakhressa pamoja na watazamaji, wasikilizaji na wafuatiliaji wa vipindi na habari mbali mbali zinazotolewa na Azam Media Limited, ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, ilieleza sehemu ya salamu za rambirambi alizozituma Dk Shein.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani Singida limesema kuwa uchunguzi wa ajali hiyo bado unaendelea. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike, alisema bado wanaendelea kumshikilia dereva wa lori lenye namba za usajili T287 DFR lililogongana uso kwa uso na gari aina ya Coaster lenye namba za usajili T 319 DMQ. Alisema taarifa kamili za chanzo cha ajali hiyo iliyotokea Jumatatu asubuhi wiki hii atazitoa wakati wowote uchunguzi utakapokamilika.

Waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni pamoja na Salim Mhando ambaye alizaliwa mwaka 1985 ambaye alikuwa mtaalamu wa kuchanganya picha, Florence Ndibalema (1989) mtaalam wa sauti, Said Haji (1989) mpiga picha, Silvanus Kassongo (1989) Injinia na Charles Wandwi (1980) mpigapicha. Wengine waliokufa kwenye ajali hiyo ni Juma Hatibu Juma (dereva wa Coaster) na Hussein Habibu.

Majeruhi katika ajali hiyo ni Mohamed Mwinshehe, Mohamed Mahige na Datus Masawe. Wafanyakazi hao wa Azam Media Limited walipoteza maisha waliagwa juzi Dar es Salaam kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Kampuni hiyo. Marehemu Salim Mhando alizikwa juzi kwenye makaburi ya Manzese- Sweetcorner jijini Dar es Salaam, Charles Wandwi alizikwa jana kwenye makaburi ya Sinza, Said Haji alizikwa juzi Hale-Tanga, Kassongo alizikwa jana mkoani Iringa na Florence Ndibalema anatarajiwa kuzikwa leo Bukoba. Watu mbalimbali akiwemo Rais Magufuli walitoa salamu za rambi rambi kufuatia msiba huo ulioikumba Azam Media Limited.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi