loader
Picha

Beyonce aachia 'ngoma' yenye Kiswahili

Staa wa muziki wa Hollywood Beyonce Knowles ‘Beyonce’ ameachia wimbo mpya wa ‘spirit’ ambao umeanza na maneno ya Kiswahili yasemayo ‘uishi muda mrefu mfalme’.

Wimbo huo ni sehemu ya albam yake mpya anayoiandaa na iliyopewa jina ‘The Lion King The Gift’ ambayo inatarajiwa kuachiwa Julai 19.

Kibao hicho kipya kipo ndani ya filamu ya Lion King inayotengenezwa na kampuni ya Disney ya nchini Marekani. Kwa mujibu wa Disney albamu hiyo imejumuisha vionjo vya waandaaji muziki kutoka barani Afrika.

Mfalme anayeimbwa kwenye wimbo huo ambaye ni moja ya wahusika wa filamu hiyo ni samba dume kijana ambaye anaanza safari ya kupambana ili kuwa mfalme wa nyika.

foto
Mwandishi: Mashirika

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi