loader
Picha

Wasichana wang'ara matokeo kidato cha sita

Watahiniwa 88,069 kati ya 91,298 waliofanya mtihani wa taifa wa kidato cha sita, 2019, wamefaulu.

Akitangaza matokeo hayo, leo Alhamis, kwenye mkutano na waandishi wa habari, Zanzibar, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) Dk Charles Msonde ameeleza kuwa mwaka huu ufaulu umepanda kwa asilimia 0.74.

“Mwaka huu ufaulu umepanda hadi kufikia asilimia 98.32 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2018 ambao ulikuwa asilimia 97.58,” aliongeza.

Ameeleza kuwa wasichana waliofaulu ni 37,219, ufaulu uliowazidi wavulana 50,850 kwa asilimia 1.07 huku ubora wa ufaulu ukiongezeka kwa kuwa na watahiniwa wengi waliofaulu kwenye daraja la 1, II, na la III.

Shule 10 bora zilizofanya vizuri zaidi kwenye mtihani huu ni pamoja na Kisimiri ya mkoani Arusha, Feza Boys ya Dar es Salaam, Ahmes ya Pwani, Mwandet wa Arusha na Tabora Boys ya Tabora.

Nyingine ni Kibaha ya Pwani, Feza Girls, ya Dar es Salaam, St. Mary’s Mazinde Juu ya Tanga, Canossa ya Dar es Salaam na Kemebos ya Kagera.

Shule 10 za mwisho kwenye mtihani huu ni pamoja na Nyambunga ya mkoani Mara, Haile Selassie na Tumekuja za Mjini Magharibi, Bumangi na Buturi za mkoani Mara na Mpendae ya Mjini Magharibi.

Nyingine ni Eckernforde ya mkoani Tanga, Nsimbo ya Katavi, Mondo ya Dodoma na Kiembesamaki ‘A’ Islamic ya Mjini Magharibi.

MAKUBALIANO ya mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ...

foto
Mwandishi: JANETH MESOMAPYA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi