loader
Picha

'Tuna mashaka kutekwa msaidizi wa Membe'

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema linaendelea kufanya uchunguzi dhidi ya tukio la utekaji kwa msaidizi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, Allan Kiluvya, ili kubaini undani wa tukio hilo kabla ya kutoa taarifa rasmi juu ya suala hilo.

Akizungumza Dar es Salaam Kamanda wa Kanda hiyo Lazaro Mambosasa amesema kimsingi tukio hilo linahitaji upelelezi wa kutosha ili kubaini kilichotokea, kutokana na kuwa na mazingira yanayotoa picha tofauti na hivyo kusababisha shaka.

“Tunaendelea na uchunguzi ili kubaini kitu kinachodaiwa kwamba mhusika alitekwa, ukiangalia clip baba mzazi alisema mtoto alipigwa sana, lakini mtoto aliposimama alisema ni mzima wa afya hajapigwa na hajateswa, lakini ukienda zaidi watekaji wamshushe wapi, wamshushe karibu na nyumbani kwa hiyo wanaongea lugha moja, mtu aliyekuteka hawezi kukushusha nyumbani,” amesema Mambosasa.

Alisema tukio hilo halina tofauti na tukio la aliyekuwa msaidizi wa Zitto Kabwe, ambaye taarifa zilisema mtu huyo alikwenda kushushwa kwa shangazi yake.

Alisisitiza kuwa kwa ujumla matukio yote hayo yanaleta shaka, hivyo kuashiria kuwa kuna ‘michezo’ ya baadhi ya watu inayohusiana na matukio hayo.

Alisema kama kweli watu hao walitekwa, upelelezi wa polisi unaoendelea, utabaini ukweli wa matukio hayo, ambayo kimsingi yanaleta shaka kutokana na kuwa na kasoro mbalimbali, zinazomfanya mtu ajiulize mara mbilimbili.

Rais John Magufuli amemuagiza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi