loader
Picha

DC kugombea jimbo la Tundu Lissu

MKUTANO Mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, umemchagua kwa kura nyingi mkuu wa wilaya hiyo, Miraji Mtaturu kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Singida Mashariki kwenye uchaguzi mdogo utakaofanyika Julai 31, mwaka huu.

Katibu Sekretarieti CCM Taifa, Salum Hatibu Reja, ambaye alikuwa msimamizi wa mkutano huo amesema DC Mtaturu amejizolea jumla ya kura 396 kati ya 600 zilizopigwa na wajumbe.

Katika mkutano huo, mwanachama Thomas Kitima alifuatia kwa kupata kura 79, Chiku Gallawa (40) wakati wagombea wengine 10 waliambulia kati ya kura moja na 17.

Mara baada ya kutangazwa kwa kinyang’anyiro cha kuwania jimbo hilo katika uchaguzi mdogo, takribani wanachama wa CCM 13 walijitokeza kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya Chama kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hivi karibuni ilitangaza Uchaguzi Mdogo katika Jimbo la Singida Mashariki mkoani hapa utakaofanyika Julai 31, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Semistocles Kaijage amesema, amefanya hivyo kutokana na barua ya Spika wa Bunge, Job Ndugai inayoeleza kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu amepoteza sifa baada ya kushindwa kuwasilisha kwake tamko la mali na madeni pamoja na kushindwa kuhudhuria mikutano saba mfululizo bila ruhusa ya Spika.

Jimbo la Singida Mashariki limekuwa chini ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambapo Lissu amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi viwili kuanzia mwaka 2010.

Rais John Magufuli amemuagiza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Abby Nkungu, Ikungi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi