loader
Picha

Simba kujichimbia Sauzi

MABINGWA wa soka Bara, Simba wanatarajiwa kuweka kambi Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

Simba inayotarajiwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, juzi ilitangaza orodha ya wachezaji 27 iliyowasajili kwa ajili ya michuano mbalimbali. Kwa mujibu wa ofisa habari wa Simba, Haji Manara, kikosi chao kinatarajiwa kwenda Afrika Kusini keshokutwa. “Wachezaji wote tuliowasajili watakuwa wameshafika kabla ya siku ya safari… na timu ikiwa kule itacheza mechi kadhaa za kirafiki,” alisema Manara.

Kwa misimu ya karibuni imekuwa utaratibu kwa baadhi ya timu kufanya kambi ya maandalizi ya msimu nje ya mji ama nchi. Msimu uliopita Simba iliweka kambi Uturuki. Mbali na Simba, wengine wenye utaratibu huo ni Yanga ambao walishawahi kuweka kambi yao Uturuki na Afrika Kusini pia, msimu huu kama ilivyokuwa msimu uliopita, wamepiga kambi yao Morogoro.

Wachezaji waliosajiliwa na Simba na ambao wanatarajiwa kwenda kambini Afrika Kusini ni Aidhi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Paschal Wawa na Erasto Nyoni. Gerson Viera, Tairone Da Silva, Wilker Da Silver, Francis Kahata, Deogratius Kanda, Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Meddie Kagere na Clatous Chama.

Wengine ni John Bocco, Mohamed Hussein,Yusuph Mlipili, Paul Bukaba, Kenedy Juma, Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael, Jonas Mkude, Rashid Juma, Miraji Athumani, Shomari Kapombe na Shiboub Sharaf.

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi