loader
Picha

Yanga yatamba kuwa moto kimataifa

KLABU ya Yanga imesema inaamini usajili wa wachezaji 26 iliofanya msimu huu utarejesha matumaini ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten amewaeleza waandishi wa habari kuwa, tayari wamemaliza usajili na sasa wanaendelea na maandalizi mkoani Morogoro.

Amesema mpaka sasa ni mchezaji mmoja wa kimataifa hajawasili ambaye ni Mnamibia Sadney Urikhob mwenye matatizo ya kifamilia, lakini atawasili wakati wowote kwa kuwa kibali chake kimeshawasili nchini.

“Kwa usajili tuliofanya ni imani tutakuwa na kikosi imara kitakachoshindana kimataifa na kutuwezesha kufanya vizuri msimu huu kuliko huko tulikotoka,” alisema.

Ten amesema wanatarajia kucheza mechi nne za kirafiki za kujipima nguvu ambapo moja itachezwa Dodoma dhidi ya Dodoma FC Julai 27, mwaka huu na tatu zitachezwa Morogoro kuanzia Julai 15, mwaka huu.

Kiongozi huyo aliwatoa hofu wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuhusu sherehe yao ya wiki ya wananchi ‘Kubwa Kuliko’akisema itafanyika isipokuwa tarehe itabadilika kutokana na kuingiliana na mechi za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndnai, Chan.

Alisema sherehe hiyo itafanyika uwanja wa taifa na kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki katika tarehe itakayotangazwa na Kamati ya Utendaji.

Katika hatua nyingine, alizungumzia maandalizi ya kikosi cha timu ya wanawake Yanga Princess akisema usajili unaendelea na tayari wameshasajili zaidi ya wachezaji 13.

Pia, kuhusu Kocha Edna Lema kutua Jangwani kwa ajili ya kuwanoa Yanga Princess alisema kuna mazungumzo yanaendelea bado hayajakamilika hivyo kama watakubaliana basi itatolewa taarifa.

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi