loader
Picha

Azam kufa, kupona Kagame

MABINGWA watetezi wa Kombe Kagame, Azam FC leo wanashuka dimbani mjini Kigali, Rwanda kuchuana na Bandari ya Kenya katika mchezo wa mwisho wa makundi utakaochezwa kwenye uwanja wa Huye.

Azam FC iliyo kundi B inahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kusonga mbele. Katika hilo litaamuliwa na matokeo ya mwisho kwa maana anayeongoza kundi ni KCCA ya Uganda yenye pointi nne, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi tatu, Bandari mbili huku Mukura ya Rwanda ikiwa na pointi moja. Mshindi kati ya Azam FC na Bandari atakuwa na nafasi ya kusonga mbele hatua ya robo fainali.

Akizungumzia mchezo huo Kocha Msaidizi wa Azam FC Idd Cheche alisema wanahitaji kuweka historia nyingine mpya kwa kuhakikisha wanapambana kufanya vizuri ili kutetea taji hilo.

“Bandari sio timu ndogo tunawaheshimu na wana wachezaji wazuri na sisi pia, tumejipanga kufanya vizuri, kikubwa kwetu tunataka kutetea taji ni lazima tupambane kupata matokeo,”alisema. Alisema ushindi utategemea na namna wachezaji wake watazingatia maelekezo ya mwalimu Ettiene Ndayiragije na kujituma uwanjani. Timu hiyo ya Chamazi inatumia mashindano hayo kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi