loader
Picha

Bangi yawekwa kwenye keki, kashata

KITENGO cha Polisi cha Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya (ADU), kimesema watumiaji wa dawa za kulevya, wamebuni mbinu mpya ya kutumia dawa hizo kwa kuweka bangi kwenye keki au kashata, hivyo wawe makini.

Aidha, kimesema kimepata taarifa kutoka kwa mwanafunzi juu ya uwepo wa matumizi dawa za vidonge vijulikanavyo kama mbandandu, ambacho hukichanganya na kinywaji cha kusisimua mwili na mtumiaji akinywa hulewa na kuwehuka.

Ofisa kutoka kitengo hicho, Ched Ngatunga alisema hayo katika banda la Jeshi la Polisi katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF), yanayotarajiwa kumalizika keshokutwa.

Alisema kutokana na kuimarishwa kwa uwepo wa matumizi ya dawa za kulevya, ndipo watumiaji wanapobuni njia za kujificha huku wakifikiri kuwa wanaweza kuendelea kutumia bila kubainika.

Alitoa mfano wa tukio la binti mmoja aliyemtembelea rafiki yake wa kiume, alipokuwa kwake alihisi njaa na alipokwenda kwenye jokofu, alikuta keki na alipokula alipoteza fahamu na kupelekwa hospitali.

“Binti huyo akiwa hospitali alipimwa na kuonekana kuwa amekula chakula chenye shida na alipozinduka aliweza kusema na waliweza kwenda kwa kijana huyo na kuikuta keki ilipopelekwa kwa mkemia mkuu ilionekana kuwa na madhara kiafya,” alisema.

Alisema tukio hilo lilitokea kati ya Machi na Aprili mwaka huu, jambo linalodhihirisha kuwa kazi ya udhibiti wa matumizi ya dawa hizo ambazo ni za kulevya zimeimarishwa.

Alisema kupitia maonesho hayo, wamepata taarifa za matumizi ya dawa za vidonge vikichanganywa na kinywaji cha kusisimua nguvu na mhusika kuwehuka na kuwa ‘chizi’.

“Mwanafunzi huyo ametufikishia taarifa hiyo hapa kwenye banda, akihoji kama mamlaka hii inafahamu uwepo wa vitendo hivyo,”alisema.

Aliongeza kuwa uelewa wa madhara ya dawa hizo, bado haujafahamika kwa kiwango kikubwa.

Alisema ni muhimu wananchi, kutokubali kupewa chakula au kitu chochote kutoka kwa asiyemfahamu hususani wawepo safarini na kukumbusha kuwa sheria zimebadilika kuanzia mwaka 2015, ambapo atakayekamatwa na bangi kuanzia kilogramu 50, hawezi kupata dhamana.

Alisema kwa dawa nyingine za kulevya, mhusika akikamatwa akiwa na zaidi ya gramu 20, adhabu yake ni kifungo cha maisha.

Rais John Magufuli amemuagiza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi