loader
Picha

Benin warejea nyumbani kishujaa

TIMU ya taifa ya Benin imeondoka juzi kutoka katika michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) bila ya kushinda hata mchezo mmoja, lakini inarejea nyumbani kama mashujaa baada ya kutolewa katika robo fainali dhidi ya Senegal.

Timu hiyo ilifanya maajabu katika fainali za mwaka huu za Mataifa ya Afrika baada ya kuifungisha virago Morocco katika hatua ya 16 bora kwa penalti, na kuibana Senegal kwa karibu dakika 70 kabla ya kufungwa bao katika dakika za mwisho na Idrissa Gueye.

“Tulikuwa na mawazo tofauti kwa kuwa tulikuwa tunafikiria kufika nusu fainali,” alisema mshambuliaji wa Benin, Steve Mounie. “Kwa upande mwingine tunajivunia lakini kwa upande mwingine, tunafikiri tungeweza kwenda mbali zaidi.” Benin ilikuwa inashiriki fainali hizo kwa mara ya nne, ilipoteza mechi nane kati ya tisa katika mashindano yaliyopita taliyofanyika mwaka 2004, 2006 na 2010, na kutoka sare nyingine.

Rekodi hiyo ina maana kuwa hawakupewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutoka katika kundi gumu ambalo lilikuwa pia na mabingwa watetezi Cameroon na vigogo wengine wa Afrika Ghana. Lakini walifanikiwa kuwabana vigogo wote hao pamoja na Guinea Bissau na kuwalazimisha sare, na kuondoka na pointi tatu na kumaliza katika nafasi ya tatu na kuwa timu mshindwa bora wa tatu na kutinga hatua ya 16 bora.

Timu hiyo ilifanya maajabu tena kwa kuiondoa Morocco kwa penalti ambayo ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kufika mbali zaidi katika michuano hiyo ya mwaka huu. Lakini Senegal ilidhihirisha umwamba wake katika mchezo huo wa robo fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa 30 June uliopo jijini hapa. “Ilikuwa safari ngumu na hapa ndio mwisho wetu,” aliongeza beki Olivier Verdon, ambaye alimpa wakati mgumu mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mane na wachezaji wenzake kabla hajatolewa dakika nane kabla ya mchezo kumalizika.

“Tunaondoka tukijivunia sana licha ya kutolewa. Tunainua vichwa vyetu juu. Kama ungetuuliza kabla ya mashindano, kama tutafikia robo fainali, wote tusingiweza kukujibu,”alisema Verdon. Kocha Michel Dussuyer, ambaye ni mzoezi wa mashindano hayo ya Mataifa ya Afrika, aliongeza: “Mashindano yametuwezesha sisi kupiga hatua mpya na kikosi changu kimeweka historia na kinastahili pongezi.”

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi