loader
Picha

Tantrade yaboresha biashara mipakani

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), imeweka mfumo katika mipaka mbalimbali ya nchi ili wafanyabiashara wa nchi za nje wakiwemo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kuzifi kia bidhaa katika mfumo ulio bora nchini.

Imesema wafanyabiashara wengi wa nje, wamekuwa wakinunua bidhaa mashambani na kwa mfumo huo itasaidia kuzikuta bidhaa hizo katika eneo moja. Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Edwin Rutageruka alisema hayo katika mkutano wa biashara ya matunda na mboga katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam(DITF) yanayoendelea katika Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Alisema Tantrade inawataka wakulima pamoja na wafanyabiashara nchini, kushirikiana nao ili kuweza kutatua changamoto ambazo wanakutana nazo katika shughuli zao.

Alisema pamoja na mikakati ya mamlaka hiyo na wadau wengine ya kuendeleza bidhaa za Tanzania, yawapasa kutoa ushirikiano wa kutosha ili kutambulisha uwezo wa ubora wa kampuni katika kufanya biashara, waweze kutambulisha uwezo na ubora wa kampuni katika kufanya biashara ili waunganishe na fursa ambazo wanazipata.

Aidha, Rutageruka alisema takwimu zinaonesha kuwa thamani ya mauzo ya bidhaa za viwandani, iliongezeka na kufikia dola za Marekani milioni 794.6 mwaka 2018 kutoka dola za Marekani milioni 693.7 mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 14.5. “Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania ina takribani viwanda 49,243 ambavyo kati yake, 393 ni viwanda vikubwa vilivyopata usajili mwaka 2016/2017.

Viwanda hivyo vilivyosajiliwa, miongoni wao vinavyozalisha bidhaa mbalimbali, ikiwemo usindikaji wa matunda na mboga lakini bado vinakabiliwa na ukosefu wa malighafi kutokana na upungufu wa uzalishaji wa ubora wa matunda, mboga, maua na viungo,” alisema. Rutageruka alisema Tanzania iko katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wa mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano wa mwaka 2016/2017- 2020/2021, unaolenga kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya Watanzania.

Rais John Magufuli amemuagiza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi