loader
Picha

Polisi yaua watuhumiwa wanne wa ujambazi

JESHI la Polisi mkoani Pwani kuwaua watu wanne ambao wanadhaniwa kuwa ni majambazi katika tukio la majibizano ya risasi huko eneo la Kwala Wilaya ya Kipolisi Mlandizi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema kuwa tukio hilo lilitokea 11/07/2019 majira ya saa 8 mchana. Nyigesa alisema kuwa baada ya kupata taarifa kuwa wapo watu wamepanga kwenda kuvamia na kupora fedha ambazo zilikuwa zimepangwa kwenda kulipwa wafanyakazi wanaojenga bandari kavu ya Kwala.

Imeelezwa kuwa Polisi waliweka mtego na majambazi hao kujikuta wakinasa.

"Baada ya kunasa na kuanzisha majibizano ya risasi na kupelekea wanne kati yao kupoteza maisha hata hivyo majambazi wawili walitoweka eneo la tukio kwa kutumia gari lingine," alisema Nyigesa.

Alisema kuwa msako wa kuwatafuta watu hao bado unaendelea ili kuwakanata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili.

"Katika tukio hilo watu hao wamekutwa wakiwa na bunduki mbili aina ya pump action, radio call, hirizi, dawa za kupulizia watu, kamba za kufungia watu, plasta za kuziba watu midomoni, leseni za udereva, vitambulisho mbalimbali vya uraia, kadi ya bima ya afya, koti, kaniki, kanzu, suruali na kaptura," alisema Nyigesa.

Aidha alisema kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi kusubiri ndugu kwa ajili ya utambuzi na kwenda kufanya mazishi.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi