loader
Picha

Majaliwa akaribisha wawekezaji wa Vietnam

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Trinh Dinh Dung na amewakaribisha wawekezaji kutoka Vietnam, waje kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo ya mipango miji, madini, bandari, usafi ri wa anga, ufundi stadi, kilimo na uvuvi.

Alisema kuwa anatambua kwamba nchi ya Vietnam inafanya vema katika suala la mazao ya kilimo kwa kuongeza tija kwenye mazao hayo na kukifanya kilimo kuwa cha biashara na kuzialika kampuni za nchi hiyo zenye teknolojia mahsusi katika maeneo tajwa ili kushirikiana na Tanzania katika mikakati yake ya kuendeleza kilimo.

Waziri Mkuu alisema hayo juzi wakati wa mkutano wake na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam na kutumia fursa hiyo kumhakikishia kwamba Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wake na nchi hiyo kwa manufaa ya watu wa nchi hizo mbili.

Alisema uwepo wa kampuni ya Viettel PLC (Halotel) ya Vietnam ni ishara tosha ya imani ya uwekezaji iliyopo kwa wawakilishi wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, kampuni ya Halotel imeweza kuzalisha ajira takriban 1,600 za moja kwa moja kwa wazawa na ajira takriban 100,000 zisizokuwa za moja kwa moja hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2018;

Akizungumzia kuhusu sekta ya utalii, Waziri Mkuu alisema Tanzania ni nchi nzuri, watu wake ni wakarimu na pia imebarikiwa vivutio vingi vya utalii, hivyo amezikaribisha kampuni za Vietnam kuja kuwekeza katika sekta ya utalii na utamaduni nchini.

Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Viet Nam, Trinh Dinh Dung aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na aliomba ushirikiano huo uimarishwe kupitia ziara za viongozi wa wakuu wa nchi mbili hizo.

Alimhakikishia Waziri Mkuu Majaliwa kuwa nchi yake, itazidi kuimarisha ushirikiano wake na Serikali ya Tanzania hususani katika sekta za kilimo, biashara na uvuvi na kuwa nchi yake iko tayari kununua mazao mbalimbali kutoka Tanzania ikiwemo korosho na pamba.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amesema katika kuhakikisha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi