loader
Picha

Kocha Simba arudi na mbwembwe

KOCHA Mkuu wa Simba Patrick Aussems ana vituko! Akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea likizo alituma salamu kuwa yuko tayari kuanza msimu mpya huku akiweka msisitizo akitumia kauli inayotumiwa na mashabiki wa timu hiyo ‘This is Simba’ (hii ndio Simba).

Katika ujumbe wake aliotuma jana kwenye mtandao wa kijamii kabla ya kutua usiku wa kuamkia leo aliandika hivi “Muda wa kurudi katika nchi nzuri ya Tanzania umewadia na niko tayari kwa msimu huu mpya, this is Simba.”

Aussems anarejea akikuta mapendekezo yake aliyoacha yamefanyiwa kazi baada ya klabu hiyo kusajili wachezaji kadhaa kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu jana alithibitisha Aussems angewasili usiku wa jana akitokea Ubelgiji ili kuanza safari ya kambi Afrika Kusini.

“Kocha atatuta usiku leo (jana) na kwenda kambini moja kwa moja kule Sea Scape kuungana na wachezaji kwa maandalizi ya mwisho tayari kwa safari ya nje ya nchi,”alisema. Rweyemamu alisema tayari wachezaji wao wamemiminika na wako katika hoteli hiyo kwani muda waliopewa wawe wamewasili wote ni jana (Jumamosi).

Kwa mujibu wa ratiba ya timu hiyo iliyotolewa juzi, jana ilikuwa siku ya wachezaji na kocha kuwasili na leo kutafanyika semina elekezi kwa wote.

Wekundu hao wa Msimbazi wanatarajiwa kuweka kambi ya wiki mbili Afrika Kusini na baadaye kurejea kwa ajili ya maadhimisho ya wiki ya Simba yanayoadhimishwa Agosti 8 ya kila mwaka.

Siku hiyo pia, hutumika kutambulisha wachezaji wake wapya iliyowasajili msimu huu tayari kwa ajili ya ligi na michuano ya kimataifa.

Wachezaji wapya waliosajiliwa ni kipa Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Ibrahim Ajibu, Gevas Fraga, Traitone Da Silva, Kenned Wilson,Deo Kanda, Wilker Henrique, Sharaf Shiboub na Francis Kahata.

BAADHI ya makocha na wachambuzi wa soka nchini ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi