loader
Picha

Yanga matamasha mtaa kwa mtaa

KABLA ya Yanga kukutana na As Vita ya DR. Congo katika kilele cha Wiki ya wananchi (Kubwa Kuliko) imepania kupita mtaa kwa mtaa na kufanya matamasha mbalimbali kupitia wasanii wa muziki na maigizo.

Yanga inataka kuwatumia wasanii ambao ni wapenzi wa klabu hiyo kurudisha hamasa kwa mashabiki wake.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wanataka wakusanye kijiji kupitia burudani hizo zitakazoenda sambamba na utoaji zawadi mbalimbali kwa wananchi.

“Wanayanga wajiandae pindi tutakapofika mitaani kwa burudani kutoka kwa wasanii pamoja na zawadi kibao zitatolewa, hakika watafurahia kile tunachotarajiwa kukifanya,” alisema.

Mipango hiyo ya mtaa kwa mtaa inatarajiwa kufanyika kuanzia wiki ijayo lengo ni kuwapa burudani wananchi kuelekea katika kilele Agosti 4, mwaka huu.

Alisema mbali na burudani wanazotarajia kutoa, watafanya shughuli nyingi za kijamii na hivi karibuni watatangaza watakapoanzia.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza Yanga inatumia ushawishi wa kiburudani wa mtaa kwa mtaa kuhamasisha wapenzi na mashabiki wake kuhusu yajayo.

Mwakelebela alisema wanataka kutumia burudani hiyo ya muziki na michezo ya kirafiki kukutana pamoja na kufurahia, kujenga ushirikiano kitu ambacho huko nyuma hakijawahi kutokea.

BAADHI ya makocha na wachambuzi wa soka nchini ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi