loader
Picha

Polisi 6 kuburuzwa kortini kwa kuomba rushwa kikongwe miaka 95

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), inatarajia kuwafikisha mahakamani askari sita wa Jeshi la Polisi na watendaji watatu wa vijiji wilayani Igunga, baada ya kuomba rushwa ya Sh milioni nane.

Akizungumza na vyombo mballimbali vya habari ofisini kwake, Kaimu Kamanda wa Takukuru mkoani Tabora, Musa Chaulo alisema kwamba watu hao watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika . Alisema kwamba watendaji hao wa serikali, walimuomba rushwa mzee Ngaka Mataluma Fale (95) baada ya kumkamata, wakimtuhumu kuwa anajihusisha na tiba asilia bila kibali, kukutwa na mfupa unaodaiwa kuwa wa binadamu, kumiliki silaha za moto, kukutwa na mafuta ya simba, ngozi ya kenge na kukutwa na bangi.

Chaulo alisema baada ya Fale kukosa kiasi hicho cha fedha, alitakiwa kuuza ng’ombe ili apate Sh milioni nane kwa ajili ya kutoa hongo kwa maofisa waliomkamata. Aliongeza kuwa Takukuru ilifanikiwa kukamata ng’ombe 11 wa Fale katika Mnada wa Igunga kwa wanunuzi, waliokuwa wakijiandaa kuwasafirisha kwenda Arusha.

Alisema baada ya kuwakamata, imewarajesha kwa mhusika. Katika hatua nyingine, Kaimu Kamanda wa Takukuru mkoani Tabora Chaulo alisema katika robo iliyoishia Juni mwaka huu, Takukuru imefuatilia na kukagua miradi 40 ya maendeleo, yenye thamani ya Sh bilioni 9.285. Alisema kati ya miradi hiyo, saba inahusu sekta ya elimu, afya na ujenzi na ina thamani ya Sh bilioni 1.570. Miradi hiyo inafanyiwa uchunguzi.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi