loader
Picha

Kilichomponza bosi wa TIB kutenguliwa na BOT hiki hapa

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesitisha uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate, Frank Nyabundege na kumteua Fred Luvanda kushika nafasi hiyo kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo, kutenguliwa kwa Nyabundege kumezingatia Kifungu Namba 33(2) na 33(2) (f) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya Mwaka 2006. Taarifa hiyo pia ilisema uteuzi wa Luvanda umezingatia Kifungu Namba 33(2)(b) cha Sheria za Mabenki na Taasisi za Fedha ya Mwaka 2006 na kuongeza kuwa hatua ya mabadiliko hayo, imetokana na mwenendo usioridhisha wa benki hiyo chini ya uongozi wa Nyabundege.

Luvanda anachukua nafasi hiyo, akitokea Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha ya benki hiyo, ambaye kwa sasa amepewa jukumu la kusimamia shughuli zote za kiutendaji za benki ya TIB Corporate.

“Hatua hizi zilizochukuliwa zina lengo la kuboresha usimamizi na utendaji wa mabenki yanayomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benki Kuu inauhakikishia umma kuwa Benki ya TIB Corporate itaendelea kutoa huduma na madai yote yaliyoiva yatalipwa kama kawaida” ilisema taarifa hiyo. Ilisema Benki Kuu itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki ili kuhakikisha sekta ya fedha inakuwa stahimilivu.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi