loader
Picha

Ndumbaro ahamasisha vita ya rushwa

NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Damas Ndumbaro amesema rushwa ni miongoni mwa sababu zinazochochea nchi nyingi za Afrika kukosa usalama na amani, kuwahimiza watanzania kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa.

Dk Ndumbaro aliyasema jijini hapa wakati wa ufunguzi wa siku Maalumu ya Mapambano dhidi ya Rushwa kwa nchi za Umoja wa Afrika. Alisema kutokana na kuwepo kwa rushwa, suala la usalama na amani katika baadhi ya nchi limekuwa tete, badala yake kumeshamiri kwa biashara ya dawa za kulevya, biashara haramu ya binadamu na ugaidi.

Dk Ndumbaro alitoa wito kwa watanzania kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki kikamilifu katika kupambana na rushwa ndani ya nchi na kutoacha vita hiyo ifanywe na rais pekee. “Hii vita si ya rais pekee, au waziri pekee yake, hii ni vita ya watanzania wote ili kuifanya nchi kuwa salama,”alisema. Alisema takwimu kuhusu upotevu wa fedha na rasilimali kupitia ripoti iliyotolewa Februari mwaka huu, zinaonesha kuwa Afrika inakadiriwa kupoteza kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.2 hadi kufikia dola za Marekani trilioni 1.4 kwa mwaka.

Dk Ndumbaro alisema pia tathmini iliyotolewa na Umoja wa Afrika mwaka 2014 inaonesha kwamba zaidi ya asilimia 25 ya Pato la Taifa (GDP) la nchi za Afrika inapotea kila mwaka na takribani dola za Marekani milioni 148 zinapotea kila mwaka kwa njia ya rushwa. Naye, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Diwani Athuman alisema taasisi yake imeokoa Sh bilioni 86 zilizotokana na watu waliojihusisha na mishahara hewa, ukwepaji kodi na makosa mengine.

Alisema pia Takukuru imefuatilia miradi ya maendeleo 1,955 yenye thamani ya zaidi ya Sh trilioni tatu, pia wamerejesha serikalini Sh bilioni 25.5 zilizotokana na urejeshwaji wa mali na fedha baada ya watuhumiwa wa rushwa kupatikana na hatia.

Akifunga siku ya mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za Umoja wa Afrika, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Mary Mwanjelwa alitoa wito kwa watanzania kuwa walinzi katika mapambano dhidi ya rushwa.

Pia alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa Bodi ya Umoja wa Afrika ya ushauri wa masuala ya rushwa kuhakikisha kila nchi mwanachama wa Umoja wa Afrika kuhakikisha inaadhimisha siku ya mapambano dhidi ya Rushwa kikamilifu. Siku maalum ya mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za Umoja wa Afrika imeenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Kuelekea kwenye Msimamo wa Pamoja wa Afrika kuhusu urejeshwaji wa Mali”.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi