loader
Picha

Mbwa wanaozurura Igunga kupigwa risasi

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Revocatus Kuuli amemwagiza Ofisa Wanyama Pori Wilaya ya Igunga, Imani Mwasongwe kuwasaka mbwa wote wanaozurura hovyo mitaani na kuwapiga risasi.

Kuuli alitoa maagizo hayo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wafugaji wa kuku, bata na mbuzi, wakilalamikia mbwa wanaozurura hovyo kuwa wamekuwa wakikamata hovyo mifugo yao pamoja na kukimbiza watu hovyo. Alisema pamoja na halmashauri kutoa matangazo kwa wilaya nzima ya Igunga ya kuwataka wafugaji wa mbwa hao, kuwapeleka kwenye chanjo pamoja na kuwafunga minyororo, baadhi yao wameshindwa kutii maagizo ya serikali huku wakijua kuacha mbwa hovyo wakizurura ni kosa.

Alisema kutokana na hali hiyo, lazima mbwa wote wanaozurura watapigwa risasi, kwa kuwa hawana wenyewe. Aliwataka wenye mbwa kuwasalimisha kwa kuwafunga mbwa wao minyororo na kuwapeleka kwenye chanjo. Baadhi ya wafugaji wa kuku, bata na mbuzi, Jumanne Mrisho, Ibrahim Lyogo na Amina Kilenga walisema hadi sasa zaidi ya kuku 21, bata 14 na mbuzi sita wameliwa na mbwa wanaozurura hovyo.

Walisema kuwa wanamshukuru mkurugenzi wa Igunga kwa kupokea kilio chao kwa kuwaua mbwa hao Ofisa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Igunga, Dk. Emmanuel Masaki alisema hadi sasa zaidi ya mbwa 39 katika Kata ya Igunga Mjini, wameuawa kwa kupigwa risasi na utararibu huo ni endelevu. Masaki alibainisha kuwa Sheria Namba 19 ya mwaka 2008 ya Ustawi wa Wanyama, inamtaka kila mfugaji wa mbwa kuwafunga mbwa mnyororo kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa nne usiku, ndipo wanaruhusiwa kuwafungulia.

Aliongeza kuwa mbwa wote watakaoendelea kuzurura, hawatabaki salama kwani wamejipanga kikamilifu na risasi wanazo za kutosha. Alisema wilaya ya Igunga ina mbwa 9,182 kwa Sensa ya mwaka 2008/2009. Ofisa Wanyamapori, Imani Mwasongwe na Ofisa Mifugo Wilaya ya Igunga, Mohamed Kiswamba walisema katika utartibu huo wa kuwapiga risasi, mbwa hao wamekuwa wakipata shida jinsi ya kuwaua mbwa hao, kwa kuwa wamekuwa wakichanganyikana kwenye makundi ya wananchi.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi