loader
Picha

SUA yaanzisha shamba mazao ya kimkakati

CHUO Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), kilichopo Morogoro kimeanzisha shamba la mazao mchanganyiko ya kimkakati kitaifa, lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kufikia uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Rasi wa Ndaki ya Kilimo chuoni hapo, Profesa Maulid Mwatawala alisema hayo mwishoni mwa wiki alipozungumza na HabariLeo kuhusu shamba la mafunzo la mfano lililoanzishwa, ambalo ni tofauti na shamba la uzalishaji la SUA ambalo limekuwepo kwa miaka mingi.

Alisema lengo la kuanzishwa kwa shamba hilo ni kuwafundisha wanafunzi na wadau mbalimbali wa kilimo kulima kilimo cha kisasa chenye tija katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025. Profesa Mwatawala alitaja mazao yanayolimwa katika shamba hilo kuwa ni mapapai ekari mbili, pesheni ekari mbili, ndizi za kupika ekari 2.6, korosho ekari sita, chikichi ekari 2.8, minazi ekari 2.7, mipera ekari moja, michungwa ekari moja, miwa nusu ekari, msimu ujao wataendelea kupanda pamoja na zabibu ekari 1.5.

Alisema kati ya mazao hayo, mazao ya kimkakati kitaifa ambayo ni chikichi, korosho na zabibu yatasambazwa katika maeneo yanayostawi ili yapatikane mavuno mengi. “Tumepanda zabibu hapa, eneo kati ya Dodoma na Morogoro hawana zao kubwa la biashara, kama zao la zabibu litafanya vizuri tutakuwa tumefungua njia kwani kwa sasa lipo kiutafiti, Serikali imepeleka korosho ukanda wa kati kuanzia Morogoro, Dodoma na Singida, hivyo kutakuwa na uhitaji mkubwa wa miche ndio maana tunajiweka sawa ili baadaye tuzalishe miche, lakini pia watu wapate eneo la kujifunza kilimo cha korosho,”alisema.

Kwa mazao yale ambayo siyo ya kimkakati kama mapapai, maembe, mapera, machungwa kama chuo wana malengo nayo kwa kuyaongezea mnyororo wa thamani katika kilimo ili yaongezewe thamani kwa kusindika ipatikane juisi, jamu na bidhaa nyingine.

Pia alisema SUA hakizalishi mazao hayo kukidhi mahitaji ila kipo kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi na wadau wa kilimo kulima kilimo cha kisasa ili wakachangie kwenye soko la ajira la taifa.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi