loader
Picha

Maelfu ya wajasiriamali vijana wajikwamua kimaisha kupitia Tigo

VIJANA ni nguvukazi muhimu, inayotegemewa na taifa, lakini tatizo kubwa linalokabili kundi hilo ni ajira. Mathalani, kwa hapa nchini inaelezwa kuwa katika vijana wenye umri wa miaka 15-34, wasiokuwa na ajira ni asilimia 13.4, ambapo wasichana ni asilimia 7.2 na wavulana ni asilimia 6.3.

Inaelezwa pia kuwa tatizo hilo la vijana kukosa ajira, linakwamisha ukuaji wa uchumi wa taifa, hasa wakati huu taifa linapoelekea kwenye uchumi wa viwanda, kutokana na vijana hao kukosa ujuzi wa kupata ajira mbalimbali na mazingira finyu ya vijana kuanzisha biashara ndogondogo. Hata hivyo, kwa miaka kadhaa sasa kampuni ya Tigo imekuwa ikibuni mbinu mbalimbali kusaidia vijana kupambana na tatizo hilo ;na mojawapo kubuni shindano kwa vijana wajasiriamali.

Katika kutekeleza hilo, Tigo inashirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali la Reach for Change kuendesha shindano la Waleta Mabadiliko ya Kidigitali wa Tigo. Shindano hilo linalenga kubaini na kusaidia wajasiriamali wa kijamii, wanaotumia vifaa vya kidijitali na kiteknolojia, kuboresha maisha na kuleta ustawi na maendeleo katika jamii. Katika shindano hilo, Tigo inatoa ruzuku kwa washiriki wa shindano hilo, ambapo washindi wa shindano hilo huingizwa katika Mkakati wa Tigo na Reach for Change.

Chini ya mkakati huo, wajasiriamali wanapewa ushauri, utaalam na kuwaunganisha na mitandao duniani, hatua inayowawezesha kujenga miradi na vitega uchumi vya kifedha endelevu, ambavyo huleta mabadiliko makubwa kwa jamii. Mwaka juzi Tigo ilitoa jumla ya dola za Marekani 40,000 kwa wajasiriamali vijana wawili, ambapo kila mmoja alipata dola 20,000. Washindi wa mwaka juzi wa shindano hilo walikuwa Sophia Mbega na Nancy Sumari.

Sophia Mbega aliwavutia majaji wa shindano hilo kwa mradi wake mkubwa wa kidijitali, unaolenga kusaidia vikundi vya kujitegemea vya wanawake vijijini vinavyojulikana kama Vicoba. Sophia alitengeneza programu ya kompyuta inayotengeneza jukwaa kwa wanawake hao kuhusu masuala ya fedha na biashara.

Programu hiyo inafaa kwa mazingira ya kiafrika, ambapo watumiaji wote, bila kujali mahali walipo, wanaweza kuhamisha fedha zao kutoka kwenye simu zao kwenda vikundi vya Vicoba moja kwa moja kwa kutumia ‘code’ maalum na kuwawezesha kuona rekodi zao za kifedha, faida wanayotengenezwa na ripoti za kila wiki. Kwa upande wake, Nancy Sumari alishinda kupitia mradi wake unaoitwa Jenga Hub unaolenga elimu ya awali kwa watoto.

Kupitia mradi huo wa Jenga Hub, Nancy alifundisha programu za kompyuta, robot na ujuzi wa ‘code’ kwa wanafunzi wa shule za msingi. Pia Jenga Hub iliwafundisha watoto hao kujifunza mambo ya msingi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), ili mwishowe kutumia teknolojia hiyo kutengeneza maudhui za elimu na burudani. “Kwa furaha tunatangaza washindi wa mwaka huu wa shindano la Waleta Mabadiliko ya Kidigitali wa Tigo. Kwa miaka mitano sasa, waleta mabadiliko wetu wamegusa maisha ya watoto 250,000 wa Tanzania.

Tuna imani kuwa kuongezeka kwa waleta mabdiliko hawa wawili, Tigo imegusa maisha ya watoto wengi zaidi nchini, hivyo kusaidia kuifanya Tanzania kuwa ni mahali salama kwa ajili ya vizazi vijavyo” alisema Diego Gutierrez, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania. Gutierrez alifafanua kuwa tigo kama chapa ya kidijitali ya maisha, inahamasisha mawazo wa teknolojia na miradi inayoleta mabadiliko endelevu.

“Teknolojia ya kidijitali, siyo tu inabadilisha jinsi tunavyofanya biashara katika Afrika, lakini inaleta mapinduzi katika jinsi tunavyopokea na kutaua changamoto za maendeleo ya kijamii. Na kwa jinsi hii tutatengeneza fursa kwa ajili ya mawazo kutambuliwa, kusaidiwa na kubadilishwa kwa ajili ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi”alisema.

Mwakajuzi ulikuwa mwaka wa tano kwa Tigo na Reach for Change, kutangaza washindi wa shindano. Washindi hao walichaguliwa kutoka kundi la maelfu ya wajasiriamali wa kijamii, wanaotumia vifaa vya kidijitali na teknolojia katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayokabili jamii za Tanzania, Gutierrez alipongeza kazi ya washindi waliopita na alihimiza Watanzania wengine kutafuta mawazo yanayofanana na hayo.

“Mpango wetu wa wajasiriamali wa kijamii unavutia mno. Hadi leo tumeweza kusaidia jumla ya waleta mabadiliko ya kidijitali 8 katika Tanzania na tunatarajia kuwasaidia wengine wengi zaidi kila mwaka’’alisema.

Waleta mabadiliko waliopo katika programu hiyo ni Faraja Nyalandu, anayeendesha mradi wa kidijitali wa kijamii unaoitwa Shule Direct. Shule Direct unatoa huduma za maudhui ya elimu kidijitali, hivyo kusaidia kuondoa tatizo la uhaba wa walimu na kuhakikisha kuwa kila kijana anapata fursa ya elimu.

Taasisi ya Faraja pia inatoa programu mtandaoni inayojulikana kama Makini SMS, inayosaidia watoto kusoma huku wakiwa na fursa ya kufanya maswali ya kuchagua kwa masomo tisa. Faraja anatarajia kusambaza taasisi yake hiyo katika nchi zingine za Afrika Mashariki. Mwingine ni Carolyne Ekyarisiima. Huyo ni Mletamabadiliko ya Kidijitali anayefanya kazi ya kuondoa pengo la kijinsia katika Tehama kupitia mradi wake wa kijamii wa Apps & Girls.

MAFUNZO ya uongozi na usimamizi wa elimu ni ...

foto
Mwandishi: Nelson Goima

Weka maoni yako

1 Comments

  • avatar
    Mjasi
    29/09/2019

    Je bado fursa ya kujiunga na mashindano ipo..? Je nawezaje kuwa mshiriki

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi