loader
Picha

TCRA sasa kutoa tuzo kwa watoa huduma

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) itaanza kutoa tuzo kwa watoa huduma za mawasiliano nchini, ikiwa ni mkakati wa kuchochea ufanisi na utoaji wa huduma za mawasiliano.

Tuzo hizo zinalenga kuongeza ushindani miongoni mwa watoa huduma, hali ambayo itaharakisha kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini kutokana na sekta hiyo. Akizungumza mjini hapa hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema tuzo hizo ni sehemu ya kutambua mchango wa watoa huduma hao.

"Mwaka huu wa fedha, TCRA imedhamiria kutoa tuzo za utaoji huduma uliotukuka katika sekta ya mawasiliano. Tunatarajia kufanya hivyo kwa sababu tunajua tuzo hizo zitahamasisha kampuni na taasisi mbalimabli kutoa ubunifu katika kuharakisha maendeleo,"alisema.

Kwa kuanzia, TCRA itatoa tuzo hizo kwa kampuni, taasisi au watu binafsi wenye mchango mkubwa kwenye sekta ya mawasiliano nchini, kabla ya kupanua wigo wa tuzo hizo katika nchi zingine kwa kushirikisha watoa huduma wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Miongoni mwa vigezo vitakavyotumika ni uwezo wa huduma zao kurahisisha shughuli za kijamii katika maisha ya kila siku ikiwemo biashara kupitia mfumo wa kidijitali.

"Sekta ya mawasiliano nchini kupitia ubunifu wa kidijitali imewezesha kampuni zinazoendesha biashara hiyo kuleta mapinduzi makubwa na kurahisisha maisha ya wananchi, hivyo kuchangia kukua kwa shughuli za kijamii na kiuchumi,"alisema.

Mkurugenzi huyo wa TCRA alisema tuzo hizo zitawafanya watoa huduma waone na kujua kufanya kazi pamoja na mamlaka hiyo mchango wao unathaminiwa na watanufaika na maboresho ya sekta hiyo pamoja na tuzo hizo ambapo ushindani utakuwa endelevu. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa EACO mjini Mwanza, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isaack Kamwelwe alisema "Sekta ya mawasiliano ni nyenzo nzuri katika kila eneo la maisha ya wananchi. Hivyo nawapongeza TCRA kubuni tuzo hizo na ningependa mimi mwenyewe nizizindue rasmi".

“Tuzo hizi zinatazamiwa kuchochea ufanisi kwa watoa huduma za mawasiliano kwa viwango vyenye ubora. Kwa miaka 20 tulikuwa hatujafikiria kuwatuza watoa huduma wetu wa sekta ya mawasiliano, kutokana na kugusa wananchi wa maeneo ya mijini na vijijini,” alieleza. Naye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliiponeza TCRA kwa mpango mkakati wao wa kutoa tuzo za utoaji huduma uliotukuka katika sekta ya mawasiliano. Alisema utoaji wa tuzo hizo kwa watoa huduma utachochea kampuni kutoa huduma zao kwa bei unafuu na kwa ushindani ili kufanya mawasiliano kuwa kichocheo cha uchumi.

MAFUNZO ya uongozi na usimamizi wa elimu ni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mwanza

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi