loader
Picha

Bil 700/- kujenga daraja Mwanza, refu zaidi EAC

Rais John Magufuli amewapa wiki moja Wakala wa Bararaba (Tanroads) na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhakikisha wamesaini mkataba, ili kuanza ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza.

Ametoa maagizo hayo leo, Jumatatu, alipokuwa akizindua huduma za tiba katika hospitali ya Bugando.

Rais Magufuli amesema kwamba serikali imetenga jumla ya bilioni 700/- kujenga daraja hili ambalo litakuwa mbadala wa usafiri wa kivuko katika eneo hilo.

“Ndani ya miezi miwili mkandarasi awe ameanza ujenzi, na daraja hili litakuwa ni refu kuliko yote kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na kati,” ameeleza.

Ameongeza kuwa daraja hilo litakuwa na urefu wa kilometa 3.2 zitakazopita majini. Upembuzi yakinifu na usanifu wa daraja hilo tayari umeshafanyika.

WILAYA ya Tunduru iliyopo mkoani Ruvuma imebarikiwa kuwa na utajiri ...

foto
Mwandishi: JANETH MESOMAPYA

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi