loader
Picha

Watano mbaroni kwa mauaji ya Watanzania

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema watu watano wamekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya Watanzania 10 nchini Msumbiji. Aidha amesema mtu mwingine mmoja ambaye naye alihusika na mauaji hayo, ametangulia mbele ya haki kwa sababu ambayo hata hivyo hakuitaja.

Aliyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa nyumba 20 za makazi ya polisi katika eneo la Magogo mjini Geita jana, ambapo Rais John Magufuli alikuwa mgeni rasmi. Watanzania hao walikufa baada ya kupigwa risasi na wengine kushambuliwa kwa mapanga na watu wanaodaiwa kuvalia sare za jeshi katika kijiji cha Mtole kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji pembezoni wa Mto Ruvuma.

Tukio hilo lilitokea Juni 26, mwaka huu ambapo mbali na mauaji hayo, pia vibanda zadi ya 30 vilichomwa moto na watu wengine wanane kujeruhiwa wakiwemo Watanzania sita na raia wa Msumbiji. Akizungumzia hatua iliyofikiwa hadi sasa mbele ya Rais Magufuli jana, IGP Sirro alisema watu hao watano ambao wamebainika kuwa walihusika na mauaji hayo tayari wametiwa mbaroni.

Mbali ya hatua hiyo IGP Sirro pia alisema Jeshi la Polisi limebaini kuwa mpango mzima wa utekelezaji wa tukio hilo la kihalifu liliandaliwa ndani ya ardhi ya Tanzania na wahusika waliingia Msumbiji ili kukamilisha tu mpango huo. “Mheshimiwa Rais napenda kukuhakikishia kuwa Jeshi la Polisi halitakubali kuona damu ya Mtanzania yeyote inapotea bure na ndio maana limekuwa linafanya kazi kubwa ili kuhakikisha kuwa linalinda maisha ya Watanzania na mali zao,” alisema IGP Sirro.

Alisema ili kuhakikisha kuwa wote waliohusika na tukio hilo wanakamatwa lakini pia ili kuhakikisha tukio kama hilo halijitokeze tena, Jeshi la Polisi linafanya operesheni ya pamoja na Jeshi la Polisi la Msumbiji ili kufikia malengo ya pamoja waliyoyapanga ili kukabiliana na matukio ya uhalifu wa kuvuka mipaka.

RAIS John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Geita

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi