loader
Picha

Safari za ATCL India ziwe chachu kukuza biashara

KAMPUNI ya Ndege za Tanzania (ATCL) imeanzisha rasmi safari mpya za ndege yake kwenda Mumbai nchini India, hatua ambayo pamoja na mambo mengine inatoa mwanya kwa wasafi ri mbalimbali wanaokwenda nchini humo kusafi ri moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwa safari tatu za kila wiki.

Jitihada za kampuni hiyo ambayo kwa kipindi kifupi tangu kufufuliwa kwake kumeonesha makusudi ya dhati ya kuleta ushindani katika sekta ya usafiri tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma. Ikumbukwe kuwa zipo nchi zikiwemo za Afrika ambazo zinamiliki ndege zake huku zikitoa huduma ya usafiri katika maeneo mbalimbali, jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine linakuza uchumi wa nchi husika pamoja na kutangaza nchi yenyewe.

Kimsingi kuanza kwa safari mbalimbali zinazofanywa na ATCL kunazidi kulitangaza taifa, ikiwa ni pamoja na vivutio vyake mbalimbali vya kitalii vilivyopo nchini zikiwemo mbuga za wanyama, misitu pamoja na Mlima wa Kilimanjaro ambao ndio mlima mrefu kushinda yote katika Bara la Afrika.

Akizungumzia kuanza kwa safari hiyo, Mkuu wa Mawasiliano wa ATCL, Josephat Kagirwa alisema safari za ndege hiyo aina ya Dreamliner 787-8 inachukua takribani saa 6 kutoka hapa nchini hadi India huku ikifanikiwa kupata mwitikio wa abiria wa kutosha kwa safari hiyo ya kwanza huku likiwa tayari limeshaanzisha safari nyingine katika nchi ya Afrika Kusini.

Ni wazi kuwa kuanza kwa safari hiyo, ni fursa kwa wafanyabiashara wa ndani ya nchi kuweza kutumia mwanya huo kwa kusafirisha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini na kuweza kutafuta katika soko nchi hiyo, jambo ambalo kwa linakuza uchumi wa nchi. Kupitia usafiri huo iwe njia ya kuwaleta wafanyabiashara kutoka India na nchi nyingine, wakiwamo hata washiriki katika maonesho mbalimbali ya kibiashara nchini.

Vilevile ikumbukwe kuwa, Tanzania inatekeleza dhana ya uchumi wa kati ambao ni wa viwanda, ambapo kwa kuwepo kwa fursa ya usafiri kama huo, ni eneo linaloweza kukaribisha wawekezaji moja kwa moja kutoka Indiana kuja nchini kuwekeza katika maeneo mbalimbali. Maendeleo ya viwanda sio tu kwamba yana uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya kilimo, ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa, lakini pia yanasaidia kuwezesha upatikanaji wa ajira katika sekta mbalimbali ambazo kwa pamoja zinaimarisha mhimili wa uchumi nchini.

Kwa fursa ya kuimarishwa kwa eneo la uchukuzi imara kutoka Tanzania hadi India, ni wazi kuwa ni njia mojawapo ya kuwavuta hata nchi jirani kuweza kutumia chombo hicho kutangaza fursa zilizopo Tanzania katika nchi wanapotoka. Kwa mantiki hiyo, Tanzania ya viwanda ni dhana yenye kuleta mabadiliko chanya yenye kukuza uchumi wa kisasa lakini pia yakiimarisha sekta mbalimbali ikiwemo za afya, elimu, kilimo, utalii na hata biashara kwa ujumla.

Kuanza kwa safari hiyo ni fahari kubwa kwa Tanzania, hivyo kampuni hiyo isiishie katika nchi hizo peke yake, lakini iwe ni moja ya eneo la kufungua milango ya anga kwa nchi nyingine na kuongeza wigo wa upatikanaji wa fursa nyingine zaidi.

KATIKA toleo hili, tunaangalia namna utamaduni uliopo katika utumishi wa ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi